Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Rais Dkt. Magufuli Aweka Mawe ya Msingi Miradi Mbalimbali Jijini Dodoma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Dodoma mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Kituo Kikuu cha Mabasi Dodoma katika eneo la Nzuguni leo tarehe 22/11/2019 jijini Dodoma. Miradi mingine ambayo Rais Mgaufuli ameweka jiwe la Msingi ni mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Uhuru Chamwino, Ujenzi wa Soko la Kisasa , Nyumba za Askari Polisi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akimtambulisha Mke wake, Mama Janeth Magufuli mbele ya wananchi wa Dodoma alipokuwa na akizungumza na wakati wa Dodoma mara baada yamara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Kituo Kikuu cha Mabasi Dodoma katika eneo la Nzuguni leo tarehe 22/11/2019 jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR –TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo akizungumza wakati wa hafla ya Uwekaji jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa Kituo Kikuu cha Mabasi katika eneo la Nzuguni jijini Dodoma leo tarehe 22/11/2019.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith Mahenge akielezea nyaraka ambazo wawekusanya kwa ajili ya utatuzi wa migogoro ya ardhi wakati wa hafla ya Uwekaji jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa Kituo Kikuu cha Mabasi katika eneo la Nzuguni jijini Dodoma leo tarehe 22/11/2019. Nyaraka hizo alimkabidhi Mhe. Rais Magufuli ili iwe rejea atakapo kutana na changamoto na malalamiko kuhusiana na migogoro ya ardhi katika jiji la Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt. John Pombe Magufuli akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith Mahenge wakati wa hafla ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Kituo Kikuu cha Mabasi Dodoma katika eneo la Nzuguni leo tarehe 22/11/2019 jijini Dodoma.

Mhe. Rais Dkt. Joseph Pombe Magufuli akisikiliza maelezo kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR –TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo kuhusu ujenzi wa Hospitali ya Uhuru inayojengwa katika wilaya ya Chamwino jijini Dodoma alipoende kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa hospitali hiyo leo trh 22/11/2019.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt. John Pombe Magufuli akipongezana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR –TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo baada ya kukata utepe kuashiria uwekaji wa jiwe lamsingi la ujenzi wa Hospitali ya Uhuru wilayani Chamwino jijini Dodoma leo tarehe 22/11/2019.Kulia ni Mke wa Rais Magufuli Mama Janeth Magufuli na kutoka kushoto ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu, Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai, na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith Mahenge.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt. John Pombe Magufuli akipongezana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma baada ya kukata utepe kuashiria uwekaji wa jiwe lamsingi la ujenzi wa Soko Kuu la Jijini Dodoma leo tarehe 22/11/2019. Mheshimiwa Rais amependekeza na kuwa jina la Soko hilo liitwe kwa heshima ya Mhe. Sipka Job Ndugai. Kutoka kushoto ni Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma, Prof. Davis Mwamfupe,Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mhe. Potabas Katambi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt. John Pombe Magufuli na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mhe. Protabas Katambi wakifunua kitamba kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa wa Soko Kuu la Jijini Dodoma leo tarehe 22/11/2019. Mheshimiwa Rais amependekeza na kuwa jina la Soko hilo liitwe kwa heshima ya Mhe. Spika Job Ndugai. Kulia ni Mke wa Mhe Rais mama Janeth Magufuli.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza mikakati ya ujenzi wa Hospitali ya Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Brigedia Charles Mbuge mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa hospitali hiyo leo tarehe 22/11/2019 jijini Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya Habari –MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi walipokutana katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi  mradi wa ujenzi wa nyumba za Askari Polisi katika eneo la Nzuguni jijini Dodoma leo tarehe 22/11/2019.

Waziri Mkuu Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne, Mhe. Mizengo Pinda akizungumza kwa niaba ya wakazi wa Dodoma wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la msingi ujenzi wa Kituo Kikuu cha Mabasi jijini Dodoma leo tarehe 22/11/2019.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Waziri Mkuu Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne, Mhe. Mizengo Pinda wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la msingi ujenzi wa Kituo Kikuu cha Mabasi jijini Dodoma leo tarehe 22/11/2019.

Picha zikionyesha muonekano wa baadhi ya sehemu za jengo la Soko Kuu la Jijini Dodoma ambalo leo tarehe 22/11/2019 Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameweka jiwe la msingi.

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, Inspekta Jenerali (IGP), Simon Sirro akimwelezea Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuhusu mradi wa ujenzi wa nyumba 118 za Askari Polisi zinazojengwa jijini Dodoma

Muoneka wa Kituo Kikuu cha Mabasi cha Dodoma ambacho leo tarehe 22/11/2019 Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa kituo hicho. (Picha zote na :Idara ya Habari – MAELEZO)

67 thoughts on “Rais Dkt. Magufuli Aweka Mawe ya Msingi Miradi Mbalimbali Jijini Dodoma

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama