Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Rais Dkt. Magufuli Kuanza Ziara ya Kikazi Visiwani Zanzibar.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam wakitokea mapumzikoni Chato mkoani Geita leo Alhamisi Januari 9, 2020

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dart es salaam mara baada ya
kuwasili akitokea mapumzikoni Chato mkoani Geita leo Alhamisi Januari
9, 2020

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 09 Januari, 2020 amewasili Jijini Dar es Salaam akitokea nyumbani kwake Chato, Mkoani Geita.

Mhe. Rais Magufuli ambaye ameongozana na Mkewe Mama Janeth Magufuli kesho ataanza ziara ya kikazi Visiwani Zanzibar ambako ataweka jiwe la msingi la jengo la Idara ya Usalama wa Taifa Zanzibar.

Keshokutwa (11 Januari, 2020), Mhe. Rais Magufuli ataweka jiwe la msingi la Shule ya Sekondari ya Mwanakwerekwe iliyopo Mjini Magharibi na atafungua hoteli yenye hadhi ya nyota tano iitwayo Hotel Verde Azam Luxury Resort and Spa iliyopo Mtoni.

Mhe. Rais Magufuli atashiriki Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 56 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar zitakazofanyika Jumapili tarehe 12 Januari, 2020 katika uwanja wa Amaan, Mjini Magharibi.

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

09 Januari, 2020

 

56 thoughts on “Rais Dkt. Magufuli Kuanza Ziara ya Kikazi Visiwani Zanzibar.

Leave a Reply to wrersewift Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *