Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Prof. Manya Atoa Maelekezo Utoaji wa Leseni kwa Viongozi wa Mgodi wa Mwime 2 Dodoma

Na. Steven Nyamiti, Dodoma

Naibu Waziri wa Madini, Prof. Shukrani Manya  amesema migogoro yote inayohusu leseni za uchimbaji madini  lazima zitatuliwe kupitia Tume ya Madini ambayo ndio taasisi yenye dhamana ya utoaji leseni hapa nchini.

Prof. Manya amewataka viongozi wa Mgodi wa Mwime 2 kufuata Sheria na Taratibu zilizowekwa na Wizara ya Madini wakati wanapohitaji leseni kwenye maeneo ya uchimbaji ili kuondoa migogoro inayojitokeza mara mara.

Ametoa maelekezo hayo leo, Januari 25. 2021 wakati alipokutana na viongozi wa Mgodi wa Mwime 2 wakiongozwa na Mwenyekiti  wa Bodi ya Wakurugenzi wa mgodi huo kutoka Kahama Mkoani Shinyanga ambapo wamefika ofisini kwake kupata maelekezo ya sababu ya ucheleweshwaji wa maombi ya leseni ya Mgodi wa Mwime 2.

24 thoughts on “Prof. Manya Atoa Maelekezo Utoaji wa Leseni kwa Viongozi wa Mgodi wa Mwime 2 Dodoma

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama