Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Prof Kikula Akagua Shughuli za Uchimbaji wa Madini na Kuhamasisha Ulipaji wa Kodi na Ufahamu wa Sheria ya Madini

Mwenyekiti wa Tume ya madini Nchini Prof Idris Kikula akifanya ukaguzi wa ulipaji wa Maduhuli wa kampuni ya Uchimbaji wa Kokoto ya Nyanza Road works alipokuwa akikagua machimbo na mitambo ya uzalishaji wa kokoto eneo la Chigongwe Jijini Dodoma.Katikati ni kamishna wa Tume ya Madini Dkt.Athanas Macheyeki na Afisa Madini wa Mkoa Bw.Jonas Mwano.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Tume ya madini nchini Prof Idris Kikula alipomtembelea kumweleze juu ya ziara yake ya kukagua Shughuli za uchimbaji wa Madini na Kuhamasisha ulipaji wa Kodi na Ufahamu wa Sheria ya Madini katika Mkoa wa Dodoma.

Makamishna wa Tume ya Madini nchini Prof Abdulkarim Mruma na Dkt.Athanas Macheyeki wakifuatilia jambo wakati walipomtembelea Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt.Binilith Mahenge leo Ofisini kwake Jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Tume ya Madini Nchini Prof Idris Kikula(mwenye kofia na miwani) akiangalia moja ya sehemu ya machimbo ya mawe leo Jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Tume ya madini Nchini Prof Idris Kikula na Kamishna wa Tume ya Madini nchini Prof Abdulkarim Mruma wakifuatilia hatua mbalimbali za uchenjuaji wa dhahabu leo Jijini Dodoma.


FacebooktwittermailFacebooktwittermail