Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Picha za Matukio Mbalimbali Fainali za AFCON U17

Mgeni Rasmi, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Juliana Shonza (kulia) akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Susan Mlawi wakati Naibu Waziri alipowasili kushuhudia fainali za mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17, jana jijini Dar es Salaam.

: Mgeni Rasmi, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Juliana Shonza (kulia) akisalimiana na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF), Bw. Ahmad Ahmad wakati Naibu Waziri alipowasili kushuhudia fainali za mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17, kati ya Guinea na Cameroon jana jijini Dar es Salaam.

Kikundi cha Mpoto Theatre kikitoa burudani kwa watazamaji wa fainali za mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 yaliyokutanisha Cameroon na Guinea hapo jana na Cameroon kutwaa ubingwa kwa mikwaju ya penati 5 dhidi ya penati 3 za Guinea.

Vikosi vya timu za vijana chini ya miaka 17 toka Guinea na Cameroon wakiimba nyimbo za mataifa yao kabla ya kuanza kwa mchezo wa fainali hapo jana ambapo Cameroon waliibuka mabingwa kwa mikwaju ya penati 5 dhidi penati 3 za Guinea.

Mgeni Rasmi, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Juliana Shonza akimkabidhi zawadi ya kombe mchezaji ambayealiibuka kuwa mfungaji bora katika mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 jana jijini Dar es Salaam.

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF), Bw. Ahmad Ahmad (katikati) akimkabidhi bendera ya CAF Balozi wa Morocco Nchini Tanzania Mhe. Abdelilah Benryane ikiwa ishara ya kuwa muandaaji wa mashindano hayo, kushoto ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Bw. Wallace Karia.

Washindi wa mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17, timu ya Cameroon wakivalishwa medali mara baada ya kuibuka na ushindi wa magoli ya penati tano dhidi ya penati tatu za Guinea jana jijini Dar es Salaam.

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF), Bw. Ahmad Ahmad akimkabidhi nahodha wa timu ya Taifa ya vijana ya Cameroon chini ya miaka 17 mara baada ya kuibuka mabingwa kwa ushindi wa magoli ya penati tano dhidi ya penati tatu za Guinea jana jijini Dar es Salaam.

Wachezaji wa timu ya Taifa ya vijana ya Cameroon chini ya miaka 17 wakishangilia mara baada ya kuibuka mabungwa wa mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 baada ya kuifunga Guinea kwa mikwaju ya penati tano dhidi ya penati tatu za Guinea jana jijini Dar es Salaam.
Picha na WHUSM – Dar es Salaam

201 thoughts on “Picha za Matukio Mbalimbali Fainali za AFCON U17

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama