Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Matukio katika Picha: Ziara ya Majaliwa Wilayani Lindi

Serikali Yatoa Bilioni 6.3 Kukarabati Vivuko Nchini

Na. Alfred Mgweno (TEMESA MTWARA)

Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, chini ya Wakala wa Ufundi naUmeme Tanzania (TEMESA) imetenga fedha kiasi cha shilingi bilioni 6.3 kwamwaka wa fedha wa 2021/2022 kwa ajili ya kuvifanyia ukarabati mkubwa vivuko nchini ambavyo vimefikia muda wake wa ukarabati.

Hayo yamebainishwa leo wakati wa mapokezi ya kivuko cha MV. MAFANIKIO kilichorejea kutoa huduma mkoani Mtwara baada ya kukamilika kwa ukarabati wake uliochukua takribani miezi miwili na nusu.

Akizunguma na wananchi waliofika kushuhudia tukio la upokeaji wa kivuko hicho lililofanyika katika eneo la Msemo Shangani Mjini Mtwara katika kivuko cha Msangamkuu – Msemo, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Brigedia Jenerali, Marco Elisha Gaguti amesema ni utaratibu wa kawaida kwa Serikali kuvifanyia vivuko ukarabati kila inapopita miaka minne hadi mitano ili kuviwezesha kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi na hivyo kivuko cha MV. MAFANIKIO wakati wake wa kufanyiwa ukarabati mkubwa ulifikia na hivyo ikawalazimu TEMESA kukiondoa ili kirejee kikiwa kiko salama na tayari kutoa huduma za kubeba abiria na mizigo.

‘’wote tunafahamu kati ya Msangamkuu na Msemo ni takribani mita 700, kwa kivuko hiki tunatumia dakika takribani tano mpaka kumi, lakini ukiondoa kivuko hiki barabara ni kilometa 29, barabara ya changarawe kutoka hapa mpaka Msangamkuu na unatumia zaidi ya saa moja mpaka saa moja na nusu kwa barabara kwa hiyo mnaweza kuona ni kiasi gani kupatikana kwa kivuko hiki baada ya matengenezo makubwa ni ukombozi mkubwa kwa wananchi wetu wa Msangamkuu katika swala la usafiri na usafirishaji’’. Alisema Mkuu wa Mkoa ambapo alimshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwezesha ukarabati huo.

Majaliwa Afungua Kongamano la Tano la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi

Kasi Uelimishaji Ugonjwa wa Uviko-19 Yazidi Kupaa

Na. Lillian Shirima: MAELEZO

Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeongeza kasi ya kutumia njia mbalimbali za kuelimisha jamii  juu ya ugonjwa  wa Uviko-19  ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa huduma ya chanjo nchini kote ili kuzuia vifo vitokanavyo na ugonjwa huo.

Afisa Program na Mratibu wa Kamati ya Maudhui, Kitengo cha Elimu ya Afya kwa Umma, Idara ya Kinga, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Bwana Saimon Nzilibili amesema hayo wilayani Bagamoyo katika Kikao Kazi kilichowakutanisha Wawakilishi wa Viongozi wa Dini kutoka Madhehebu yote.

Washiriki wengine ni kutoka Taasisi za Kiserikali na Wadau wa Maendeleo na Huduma za Afya kutoka WHO, UNICEF na Family Heath International (FHI) ambao kwa pamoja wamekutana kuandaa nyenzo maalum zitakazotumiwa na viongozi wa Dini nchini kutoa taarifa kwa waumini wa dini zote kuhusu ugonjwa wa Uviko-19 upatikanaji wa chanjo kama njia ya kujikinga maabukizi ya ugonjwa huo.

“Tunaendelea kuhakikisha makundi mbalimbali ya watanzania yanafikiwa kwa kutumia mbinu tofauti, matangazo ya radio, televisheni, magazeti na mitandao ya kijamii na sasa hii nyenzo (bango kitita) inayoandaliwa ni kwaajili ya viongozi wa Dini’.

Majaliwa Azungumza na Mabalozi Watakaoiwakilisha Tanzania Katika Nchi Mabalimbali

ev eşyası depolama