Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Taarifa ya Utekelezaji wa Sheria ya Mazingira Yawasilishwa kwa Kamati ya Bunge

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Sima akifafanua jambo mbele ya Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira mara baada ya kuwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Sheria ya Mazingira katika ngazi ya Serikali za Mitaa. Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Balozi Joseph Sokoine akifuatilia majadiliano mara baada ya Ofisi yake kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Sheria ya Mazingira mbele ya Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira. Kulia ni Mhe. Hawa Mwaifunga Mbunge wa Viti Maalumu.

Sehemu ya waheshiwa wabunge wakifuatilia mjadala, kulia ni Mhe Josephine Genzabuke na Mhe. Gibson Blasius Meiseyeki.

45 thoughts on “Taarifa ya Utekelezaji wa Sheria ya Mazingira Yawasilishwa kwa Kamati ya Bunge

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *