Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

NEC Yakanusha kutoa Ratiba ya Uchaguzi Mkuu 2020

Na. Immaculate Makilika – MAELEZO
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imekanusha kutoa ratiba ya Uchaguzi Mkuu
unaotarajiwa kufanyika mwaka huu, na kuwataka wananchi kupuuza taarifa
inayosambaa kwenye mitandao kwani si taarifa rasmi na imeandaliwa kwa nia ovu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyolewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa tume hiyo Dkt.
Wilson Charles inaeleza kuwa taarifa hiyo potofu inayosambazwa kupitia
mitandao ya kijamii hasa What sApp.

“Tume ya Taifa ya Uchaguzi, kwa kujibu wa Ibara ya 74(6)(b) na (d) ya Katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, imepewa mamlaka ya
kusimamia na kuratibu uendeshaji wa Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani.
Katika kutekeleza jukumu hilo, kifungu cha 35B cha Sheria ya Uchaguzi, sura ya
292, kinaipa NEC mamlaka ya kutangaza katika gazeti la Serikali tarehe ya
Uchanguzi” alisema Dkt. Charles.
Aliongeza kuwa, mamlaka hayo yanatekelezwa kwa mujibu wa kifungu cha 37(1)
(a) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, sura ya 343 ambacho kinailekeza NEC
kutangaza tarehe ya uchaguzi mara baada ya Bunge kuvunjwa.
Aidha, kwa kuwa Bunge halijavunjwa, NEC haijatoa wala kutangaza ratiba yoyote
ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.

FacebooktwittermailFacebooktwittermail