Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Azuru Hifadhi ya Saadani

1. Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (katikati) akioneshwa ramani ya Hifadhi ya Taifa ya Saadani na Mwakilishi wa Mkuu wa Hifadhi za Taifa, Vitalis Kuluka huku akishirikiana kuonesha eneo hilo na Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo,Erica Yigella ( wa pili kulia) mahali kilipo Kitongoji cha Uvinje ambapo wakazi wa eneo hilo wamegoma kuhama ndani ya hifadhi hiyo na wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea hifadhi hiyo jana. Wa kwanza kulia ni Afisa Wanyamapori, Godfrey Maro na Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Saadani, Stephano Msumi na pande wa kulia nyuma ya Katibu Tawala ni Msaidizi wa Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa, Fredrick Mofulu

2. Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga ( wa pili kulia ) akizungumza na Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Saadani , Stephano Msumi ( katikati) wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea hifadhi hiyo jana kwa ajili ya kujionea changamoto mbalimbali zinazoikabili . Wa kwanza kulia ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo, Erica Yigella, Wa kwanza kushoto ni Mwakilishi wa Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Vitalis Kuluka, wa tatu kushoto ni Msaidizi wa Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa, Fredrick Mofulu

3. Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akizungumza jana na Wananchi wa Kitongoji cha Uvinje ambao wamegoma kuhama ndani ya hifadhi hiyo, wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea kwa ajili ya kuzungumza nao ili kujua ukubwa tatizo la mgogoro huo uliodumu kwa zaidi ya miaka 10 sasa .

4. Bango lililopo katika geti la Gama linalokuelekeza sheria na taratibu ukiwa unaingia katika Hifadhi ya Taifa ya Saadani iliyopo wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.

5. Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga ( kushoto ) akipatiwa maelezo na Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Saadani , Stephano Msumi ( katikati) wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea hifadhi hiyo jana kwa ajili ya kujionea changamoto mbalimbali zinazoikabili .Wa kwanza kulia ni Mwakilishi wa Mkuu wa Hifadhi ya Taifa, Vitalis Kuluka, nyuma ya Mhifadhi wa Saadani ni Msaidizi wa Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa, Fredrick Mofulu

6. Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga ( mbele ) akiwa na baadhi ya viongozi wa Hifadhi za Taifa pamoja kamati ya ulinzi na usalama kutoka Wilayani Bagamoyo akiongoza kwenda kuangalia sehemu kunakofanyika utalii wa boti katika Hifadhi ya Taifa ya Saadani wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea hifadhi hiyo jana kwa ajili ya kujionea changamoto mbalimbali zinazoikabili .

7. Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (wa pili kulia) akipatiwa maelezo na Msaidizi wa Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa, Fredrick Mofulu ( wali kushoto) kuhusiana na sehemu kunakofanyika utalii wa boti katika Hifadhi ya Taifa ya Saadani . Wengine ni baadhi ya viongozi wa Hifadhi za Taifa pamoja na kamati ya ulinzi kutoka Wilayani Bagamoyo . (Picha na Lusungu Helela)

FacebooktwittermailFacebooktwittermail