Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Naibu Waziri Shonza Aridhishwa na Maboresho ya Uwanja wa Nyamagana

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza akishika nyasi bandia za Uwanja wa Nyamagana wakati alipotembelea kujionea maendeleo ya ukarabati wa uwanja huo jana jijini Mwanza.

Sehemu ya Uwanja wa mpira wa miguu wa Nyamagana jijini Mwanza.

Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza Mhe. Bikhu Kotecha akielezea changamoto zinazoikabili Halmashauri hiyo katika kufanikisha ujenzi wa Uwanja wa Nyamagana (kushoto) wakati Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza (katikati) alipotembelea kujionea maendeleo ya ukarabati wa uwanja huo jana jijini Mwanza kulia ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Nyamagana Alfred Madulu.

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza (katikati) akifafanua jambo kwa viongozi na wadau wa mpira wa miguu wakati alipotembelea kujionea maendeleo ya marekebisho ya Uwanja wa Nyamagana jana jijini Mwanza, kulia ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Nyamagana Alfred Madulu na kushoto ni Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza Mhe. Bikhu Kotecha.


FacebooktwittermailFacebooktwittermail