Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Naibu Waziri Nishati Awaonya Wakandarasi Wanaosuasua


Na Hafsa Omar – Katavi 

Naibu waziri wa Nishati, Subira Mgalu amesema Serikali haitasita kusitisha mkataba wa Mkandarasi yoyote ambae ataonekana kusuasua katika kutekeleza majukumu yake na kwenda kinyume na mkataba waliokubaliana nao.

Ameyasema hayo, Julai 7, 2020, wakati alipokuwa akizungumza wa wananchi wa kijiji cha Kenswa Nsimbo, kata ya Katumba,Wilaya ya Mpanda,mkoani Katavi, kabla ya kuwasha umeme kwenye kijiji hicho.

Naibu Waziri aliyasema hayo baada ya kutoridhishwa na kasi ya usambazaji umeme na kampuni ya China Railway Construction Electrification Bureau Group Co Ltd( CRCEBG) iliyopewa kazi ya usambazaji umeme mkoani humo.

One thought on “Naibu Waziri Nishati Awaonya Wakandarasi Wanaosuasua

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *