Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar aitembelea Tanzania

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar, Mhe. Mohammed Bin Abdulrahman Al-Thani, amewasili nchini na kupokelewa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe, jana tarehe 20 Machi, 2019. Mhe. Al-Thani atakuwa nchini kwa siku moja ambapo atakutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, kabla ya kuondoka kuelekea Rwanda

Sehemu ya ugeni huo ukiwasili.

Wajumbe wa msafara huo wakisalimiana na viongozi wa serikali waliofika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, kuwapokea akiwemo Balozi wa Tanzania nchini Qatar Mhe. Fatma Mohammed Rajab na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Ayoub Mndeme.

 

 


FacebooktwittermailFacebooktwittermail