Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Naibu Waziri Mabula Aibukia Kanisani na Kuhimiza Ulipaji Kodi ya Ardhi

Na Munir Shemweta, SONGWE

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angeline Mabula ameibuka katika kanisa Katoliki Parokia ya Mwambani katika kata ya Mkwajuni wilayani Songwe na kuwahimiza waumini wa kanisa hilo kuhakikisha wanalipa kodi ya pango la ardhi.

Akizungumza na waumini wa kanisa hilo jana akiwa katika ziara yake ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi kwenye mkoa wa Songwe Dkt. Mabula alisema, wamiliki wote wa ardhi nchini wanapaswa kulipa kodi ya pango la ardhi ili kuongeza mapato na kuiwezesha Serikali   kuwatumikia wananchi katika shughuli za maendeleo.

Aliwaeleza waumini wa kanisa Katoliki Parokia ya Mwambani kuwa, ardhi ni mali na mtaji na katika kuitunza lazima iongezwe thamani kwa kupangwa, kupimwa na kumilikishwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama