Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Naibu Waziri Dkt. Mollel Awasili Ofisini Kwake Mtumba.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Godwin Oloyce Mollel akitia saini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili ofisini kwake Mtumba Jijini Dodoma leo tarehe 21 Mei, 2020 baada ya kuapishwa kushika nafasi hiyo.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Godwin Oloyce Mollel akisalimiana na watumishi wa Wizara hiyo mara baada ya kuwasili ofisini kwake Mtumba Jijini Dodoma leo tarehe 21 Mei, 2020 baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kushika nafasi hiyo. Wa pili kushoto ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu. Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW


FacebooktwittermailFacebooktwittermail