Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Naibu Waziri Biteko Asisitiza Matumizi ya Vifaa vya Usalama Mahali pa Kazi

Naibu Waziri wa Madini, Mhe. Dotto Biteko akizungumza na wachimbaji wadogo wa madini ya Jasi wakati wa kikao baina yake na wachimbaji hao jana katika eneo la Makanya wilayani Same mkoa wa Kilimanjaro. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Same, Bi. Anne Claire Shija , Katibu Tawala wa Wilaya ya Same, Bw.Sospeter Mabenga na Afisa Madini wa Mkoa wa Kilimanjaro Bi. Fatma Kyando.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro akizungumza wakati wa kikao baina ya Naibu Waziri wa Madini, Mhe. Dotto Biteko (kulia) na wachimbaji wadogo wa madini ya Jasi katika eneo la Makanya wilayani Same mkoa wa Kilimanjaro alipofanya ziara katika machimbo hayo jana.

Naibu Waziri wa Madini, Mhe. Dotto Biteko akizungumza na wafanyakazi wa mgodi wa madini ya Jasi (Gypsum) alipofanya ziara katika eneo la uchimbaji wa madini hayo lililopo Makanya, Same mkoani Kilimanjaro jana.

Naibu Waziri wa Madini Mhe. Dotto Biteko akitembelea eneo la uchimbaji wa madini ya Jasi (Gypsum) lililopo Makanya, Same mkoani Kilimanjaro jana tarehe 09/10/2018.

Naibu Waziri wa Madini, Mhe. Dotto Biteko akisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa Afisa Madini wa Mkoa wa Kilimanjaro Bi. Fatma Kyando (kushoto) wakati wa ziara yake katika eneo la uchimbaji wa madini Jasi (Gypsum) lililopo Makanya, Same mkoani Kilimanjaro jana.

Madini ya Jasi (Gypsum) yakiwa tayari baada ya kuchimbwa katika eneo la uchimbaji wa madini hayo lililoko Makanya, Same mkoani Kilimanjaro.Madini haya utumika kama mali ghafi katika viwanda vya Simenti.

Naibu Waziri wa Madini, Mhe. Dotto Biteko akitazama eneo la uchimbaji wa madini ya Jasi (Gypsum) lililopo Mkanya, Same mkoani Kilimanjaro wakati wa ziara yake katika eneo hilo jana. (Picha zote na Idara ya Habari – MAELEZO, Same)


FacebooktwittermailFacebooktwittermail