Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Na Mathias Canal, WEST-Dodoma

Wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi wa Chama cha SKAUTI Tanzania wakifuatilia hotuba ya Mgeni rasmi-Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prof Adolf Mkenda wakati akifungua mkutano huo tarehe 2 Julai 2022 katika ukumbi wa Chuo cha Mipango Jijini Dodoma.
Mlezi wa SKAUTI ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan ana matumaini na matarajio makubwa kwa Chama cha SKAUTI nchini kuwa eneo muhimu la malezi na ukakamavu kwa vijana.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda ameyasema hayo tarehe 2 Julai 2022 katika ukumbi wa Chuo cha Mipango Jijini Dodoma wakati akifungua mkutano mkuu wa uchaguzi wa Chama cha SKAUTI Tanzania.
Waziri Mkenda ametoa salamu za Rais Samia mbele ya wajumbe hao na kuwakumbusha kuwa uchaguzi huo unapaswa kuwa kielelezo cha uchaguzi wa viongozi bora wenye weledi, nidhamu na mshikamano miongoni mwao.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof Adolf Mkenda akisistiza jambo wakati akifungua mkutano mkuu wa uchaguzi wa Chama cha SKAUTI Tanzania tarehe 2 Julai 2022 katika ukumbi wa Chuo cha Mipango Jijini Dodoma.

60 thoughts on “Na Mathias Canal, WEST-Dodoma

Leave a Reply to FifineOnPn Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama