Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Mwaka 2024 Tanzania Kuzalisha Tani 672,000 za Sukari

Na Immaculate Makilika – MAELEZO

Akizungumza leo jijini Dodoma, Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO na  Msemaji Mkuu wa Serikali, alisema kuwa wa sasa juhudi kubwa zimeelekezwa katika kuongeza uzalishaji katika viwanda vya sukari  vilivyopo Kagera, Mtibwa na Kilombero pamoja na kuhamasisha kuanzishwa kwa mashamba na viwanda vipya vitakavyozalisha sukari nchini.

Msigwa alisema kuwa katika kipindi cha miaka mitatu ijayo viwanda vya sukari vya Kagera, Mtibwa na Kilombero vinatarajia kuongeza uzalishaji wa tani 265,000, ambazo zitaongezeka kwenye tani 367,000 zinazozalishwa sasa.

Alibainisha kuwa wawekezaji wapya wa  Bagamoyo Sugar wameshalima shamba na tayari wamefunga mitambo  Bagamoyo mkoani Pwani ambapo wanatarajia kuzalisha sukari kuanzia mwezi Juni mwaka 2022 wakianza na tani 20,000 na baadaye kuzalisha zaidi ya tani 50,000 katika kipindi cha  miaka mitatu ijayo.

37 thoughts on “Mwaka 2024 Tanzania Kuzalisha Tani 672,000 za Sukari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama