Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Msemaji Mkuu wa Serikali Apiga Kura, Asifu Amani, Utulivu Dodoma Jiji


Na Mwandishi Wetu-MAELEZO
Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, amekamilisha haki yake ya kikatiba kwa kupiga kura katika eneo la Kilimani, jijini Dodoma.
Katika eneo hilo ambapo pia awali na baadaye walionekana viongozi wengine mbalimbali wa Serikali, Chama na taasisi binafsi, Dkt. Abbasi alikaa kwenye foleni kama kawaida na wananchi wengine na alipomaliza kupiga kura akasisitiza:
“Nimekamilisha haki yangu ya kikatiba kwa furaha sana kwa sababu tukiwa pale kwenye foleni tunapiga stori za hapa na pale wananchi walikuwa wanasema sio wote tuliopiga nao kura mwaka 2015 leo wamepata bahati tena kama hii kwa maana ya uhai kushiriki nasi. Hivyo ni jambo si tu la kikatiba lakini lenye hisia kubwa kibinadamu na kiroho mtu anapolitimiza.”

7 thoughts on “Msemaji Mkuu wa Serikali Apiga Kura, Asifu Amani, Utulivu Dodoma Jiji

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama