Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Mkuu wa Wilaya Ikungi Akunwa na Maonesho ya Siku ya Chakula Duniani

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Kilimo, Bw. Revocatus Kasimba akifafanua jambo mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Bw. Edward Mpogolo (kulia) alipotembelea katika maonesho ya bidhaa za chakula na lishe yanayoendelea katika viwanja vya Bomberdier mjini Singida leo ikiwa ni maadhimisho ya siku ya chakula dunia ambayo kitaifa inafanyika mkoani Singida na ambapo kilele chake itakuwa tarehe 16 Oktoba 2019. Kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Kilimo, Mbaraka Omari na Mratibu wa maonesho hayo Sadoti Makwaruzi.

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Bw. Edward Mpogolo akipata maelezo namna ya unga wa lishe utokanao na maharage kutoka kwa Mtafiti wa Maharage toka Taasisi ya Utafiti ya Kilimo (TARI) Kituo cha Seliani Arusha, Bi. Editha Kadege alipokuwa akitembelea mabanda katika maonesho ya bidhaa za chakula na lishe yanayoendelea katika viwanja vya Bomberdier mjini Singida ikiwa ni maadhimisho ya siku ya chakula dunia ambayo kitaifa inafanyika mkoani Singida na ambapo chake itakuwa tarehe 16 Oktoba 2019

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Bw. Edward Mpogolo akiwekewa uji uliopikwa kwa kutumia unga lishe utokanao na maharage kutoka kwa Mtafiti Msaidizi toka Taasisi ya Utafiti ya Kilimo (TARI) Kituo cha Seliani Arusha, Bibi. Dimetria Mugo alipokuwa akitembelea mabanda katika maonesho ya bidhaa za chakula na lishe yanayoendelea katika viwanja vya Bomberdier mjini Singida ikiwa ni maadhimisho ya siku ya chakula dunia ambayo kitaifa inafanyika mkoani Singida na ambapo chake itakuwa tarehe 16 Oktoba 2019.

Mtafiti wa Maharage toka Taasisi ya Utafiti ya Kilimo (TARI) Kituo cha Seliani Arusha, Bi. Editha Kadege akiwaelezea wanafunzi wa shule ya Sekondari Salimin ya mjini Singida namna unga wa lishe utokanao na maharage unavyotengenezwa walipotembelea banda la TARI leo katika maonesho ya bidhaa za chakula na lishe yanayoendelea katika viwanja vya Bomberdier mjini Singida ikiwa ni maadhimisho ya siku ya chakula dunia ambayo kitaifa inafanyika mkoani Singida na ambapo chake itakuwa tarehe 16 Oktoba 2019.

Mtafiti toka Taasisi ya Utafiti ya Kilimo Tanzania(TARI) Makao Makuu Dodoma, Bibi. Mshaghuley Ishika akiwaelezea wanafunzi wa shule ya Sekondari Salimin ya mjini Singida kuhusu usindikaji wa zabibu za mezani walipotembelea banda la TARI leo katika maonesho ya bidhaa za chakula na lishe yanayoendelea katika viwanja vya Bomberdier mjini Singida ikiwa ni maadhimisho ya siku ya chakula dunia ambayo kitaifa inafanyika mkoani Singida na ambapo chake itakuwa tarehe 16 Oktoba 2019.(Pichana Idara ya Habari –MAELEZO)

One thought on “Mkuu wa Wilaya Ikungi Akunwa na Maonesho ya Siku ya Chakula Duniani

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama