Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Mkurugenzi Msigwa, Mkurugenzi Oparah Wakubaliana Kuwajengea Uwezo Maafisa Habari/Uhusiano Kufanya Kazi Zitakazoitangaza Vyema Afrika

Na Mwandishi Wetu – Dar es Salaam.


Mkurugenzi wa Idara ya Habari -MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Bw. Gerson Msigwa amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Afrika, Bw. Emeka Oparah kando ya Mkutano wa 33 wa Maafisa Uhusiano Barani Afrika (APRA) unaoendelea Katika ukumbi wa JINCC Jijini Dar es Salaam.


Katika mazungumzo hayo, Msigwa na Oparah wamekubaliana kuongeza ushirikiano kati ya Airtel na Wadau wa Mawasiliano wa Tanzania kwa kuwa na mipango ya kujenga uwezo kwa Maafisa Habari na Uhusiano ili kuwawezesha kufanya kazi zitakazoitangaza vyema Afrika na kukuza fursa za haki ya kupata taarifa.


Pia, wamezungumzia baadhi ya changamoto zinazowakabili Maafisa Mawasiliano na Uhusiano ambazo zinahitaji majawabu kutoka kwa wadau mbalimbali zikiwemo Serikali.

50 thoughts on “Mkurugenzi Msigwa, Mkurugenzi Oparah Wakubaliana Kuwajengea Uwezo Maafisa Habari/Uhusiano Kufanya Kazi Zitakazoitangaza Vyema Afrika

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama