Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

MKURABITA Yasogeza Huduma za Urasimishaji kwa Wananchi

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Simiyu ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Bw. Festo Kiswaga akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Vituo Vya Kurasimisha na Kuendeleza Biashara kwa Kanda ya Ziwa Mashariki jana Mjini Bariadi. Vituo hivyo vitakuwa vikitoa huduma za urasimishaji biashara kwa kuwepo wataalamu wote wanaohusika na usajili na utoaji huduma za uanzzishaji na uendelezaji wa biashara kama vile Brella, TRA, Afisa Biashara, Wakala wa Vipimo, taasisi za kibenki na sekta binafsi inayowakilishwa na Kampuni ya GODTEC.

Na: Mwandishi Wetu, Bariadi

Waziri wa Nchi  Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Kapteni Mstaafu George Mkuchika ameziagiza  halmashauri zote nchini  kutenga maeneo ya uanzishwaji vituo vya urasimishaji biashara kwa wananchi ili waweze kuondokana na umasikini.

Agizo hilo limetolewa na kwa naiba yake na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Festo Kiswaga  katika uzinduzi wa kituo kimoja cha urasimishaji na uendelezaji biashara katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Amesema MKURABITA ndio nyenzo muhimu ya kuwawezesha, kuibua na kuendeleza uwezo wa wananchi kuwa wawekezaji wa ndani wanaowajibika kutengeneza mtaji, soko, ajira na kujenga uchumi wa viwanda ndani ya mfumo rasmi, hivyo ipo haja kwa halmashauri kutenga maeneo kwa ajili ya vituo vya urasimishaji biashara  ili kuwasaidia wananchi.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya GODTEC Paul Chizi akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kituo kimoja cha Kurasimisha na Kuendeleza Biashara kwa Kanda ya Ziwa Mashariki leo Mjini Bariadi. Vituo hivyo vitakuwa vikitoa huduma za urasimishaji biashara kwa kuwepo wataalamu wote wanaohusika na usajili na utoaji huduma za uanzzishaji na uendelezaji wa biashara kama vile Brella, TRA, Afisa Biashara, Wakala wa Vipimo, taasisi za kibenki na sekta binafsi inayowakilishwa na Kampuni ya GODTEC.

Mratibu wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) akisisitiza jambo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kituo kimoja cha Kurasimisha na Kuendeleza Biashara kwa Kanda ya Ziwa Mashariki jana Mjini Bariadi. Vituo hivyo vitakuwa vikitoa huduma za urasimishaji biashara kwa kuwepo wataalamu wote wanaohusika na usajili na utoaji huduma za uanzzishaji na uendelezaji wa biashara kama vile Brella, TRA, Afisa Biashara, Wakala wa Vipimo, taasisi za kibenki na sekta binafsi inayowakilishwa na Kampuni ya GODTEC.

  “ Ni matumaini yangu kuwa vituo vya kurasimisha biashara vitatumika pia kutambua na kuzitumia fursa za uwekezaji ambazo zinatengenezwa na kuimarishwa, nitumie fursa hii kuzitaka Halmashauri zote nchini kutenga maeneo kwa ajili ya uanzishwaji wa vituo hivi katika kuchochea ujenzi wa uchumi wa viwanda vinavyomilikiwa na wananchi” alisema Kiswaga akisoma hotuba ya Waziri Mkuchika .

Aidha, amewahamasisha wafanyabiashara na wananchi wote mkoani Simiyu kutumia huduma zipatikanazo katika vituo vya kusajili na kuendeleza biashara zao, huku akiwasisitiza wafanyabiashara wadogo kama mamalishe, wamachinga na waendesha bodaboda kutumia Kituo cha Bariadi, ili waweze kujiondoa katika mfumo usio rasmi na kuingia katika mfumo rasmi wa uchumi.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya MKURABITA Balozi Daniel Ole Njoolay ameiomba Serikali kutoa nyenzo za kutosha za kusukuma urasimishaji na uendelezaji wa biashara kukuza mitaji ya wafanyabiashara kwa kuwa hadi sasa utafiti unaonesha kuwa kuwa zaidi ya asilimia 90 ya biashara si rasmi.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Simiyu ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Bw. Festo Kiswaga (wa nne kutoka kushoto) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Kituo Kimoja cha Urasimishaji na Uendelezaji wa Biashara kwa Kanda ya Ziwa Mashariki kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo jana Mjini Bariadi. Vituo hivyo vitakuwa vikitoa huduma za urasimishaji biashara kwa kuwepo wataalamu wote wanaohusika na usajili na utoaji huduma za uanzishaji na uendelezaji wa biashara kama vile Brella, TRA, Afisa Biashara, Wakala wa Vipimo, taasisi za kibenki na sekta binafsi inayowakilishwa na Kampuni ya GODTEC. Kutoka kulia ni mjumbe wa MKURABITA Bibi. Anna Mwasha, Mratibu wa MKURABITA Bibi. Seraphia Mgembe, Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Kapteni mstaafu John Chiligati, Mwenyekiti mpya wa Kamati ya MKURABITA, Balozi Daniel Ole Njolay,Mkuu wa Wilaya ya Urambo Angelina Kwingwa na na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Merkizedeck Humbe.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Simiyu ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Bw. Festo Kiswaga akipeana mkono na msoma risali kwa niaba ya wanufaika wa mafunzo ya MKURABITA Bw. Erimlingi Kimaro wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kituo Kimoja cha Urasimishaji na Uendelezaji wa Biashara kwa Kanda ya Ziwa Mashariki leo Mjini Bariadi. Vituo hivyo vitakuwa vikitoa huduma za urasimishaji biashara kwa kuwepo wataalamu wote wanaohusika na usajili na utoaji huduma za uanzishaji na uendelezaji wa biashara kama vile Brella, TRA, Afisa Biashara, Wakala wa Vipimo, taasisi za kibenki na sekta binafsi inayowakilishwa na Kampuni ya GODTEC.

Mwenyekiti Mstaafu wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) Kapteni mstaafu John Chiligati ametoa wito kwa wakazi wa Mkoa wa Simiyu hususani Bariadi kutumia hati miliki za kimila kama dhamana ya kupata mikopo ya kuendeleza kilimo, kuanzisha viwanda na biashara.

Mratibu wa MKURABITA Seraphia Mgembe amewashukuru wote waliopata mafunzo ya urasimishaji na uendelezaji wa biashara na kuahidi kuwafuatilia na kuhakikisha kuwa miaka ijayo waweze kufanikiwa kiuchumi.

Baadhi ya washiriki wa Mafunzo ya urasimishaji na uendelezaji wa biashara wameishukuru Serikali kwa mpango huo kuanzisha mradi wa kituo kimoja cha urasimishaji na uendelezaji biashara, kupitia MKURABITA na kuomba waendelee kupewa mafunzo ili wawze kunufaika na biashara zao.

“Tunaomba tuendelee kupigwa msasa zaidi na zaidi ili tuweze kutunza mahesabu ya biashara zetu vizuri, tuweze kulipa kodi na kuendeleza biashara zetu katika mfumo ulio rasmi” alisema Mashaka Than mfanyabiashara kutoka Bariadi.

Baadhi ya wanufaika wa mafunzo kuhusu urasimishaji wakifuatilia hotuba ya viongozi mbalimbali wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kituo Kimoja cha Urasimishaji na Uendelezaji wa Biashara kwa Kanda ya Ziwa Mashariki leo Mjini Bariadi. Vituo hivyo vilivyobuniwa na MKURABITA kwa kushirikiana na Kampuni ya GODTEC  vitakuwa vikitoa huduma za urasimishaji biashara kwa kuwepo wataalamu wote wanaohusika na usajili na utoaji huduma za uanzzishaji na uendelezaji wa biashara kama vile Brella, TRA, Afisa Biashara, Wakala wa Vipimo, taasisi za kibenki na sekta binafsi inayowakilishwa na Kampuni ya GODTEC.

Mkuu wa Wilaya ya Urambo mkoani Tabora, Bibi. Angelina Kwingwa akiteta jambo na Mwenyekiti wa MKURABITA aliyemaliza muda wake Kapteni mstaafu John Chiligati walipokutana katika hafkla ya uzinduzi wa Kituo Kimoja cha Urasimishaji na Uendelezaji wa Biashara kwa Kanda ya Ziwa Mashariki jana Mjini Bariadi. Vituo hivyo vilivyobuniwa na MKURABITA kwa kushirikiana  a Kampuni ya GODTEC vitakuwa vikitoa huduma za urasimishaji biashara kwa kuwepo wataalamu wote wanaohusika na usajili na utoaji huduma za uanzzishaji na uendelezaji wa biashara kama vile Brella, TRA, Afisa Biashara, Wakala wa Vipimo, taasisi za kibenki na sekta binafsi inayowakilishwa na Kampuni ya GODTEC.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Simiyu ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Bw. Festo Kiswaga akiweka saini katika kitabu cha wageni katika Ofisi za Kituo Kimoja cha Urasimishaji na Uendelezaji wa Biashara mara baada ya kuzindua rasmi kituo hicho jana mjini Bariadi. Vituo hivyo vitakuwa vikitoa huduma za urasimishaji biashara kwa kuwepo wataalamu wote wanaohusika na usajili na utoaji huduma za uanzzishaji na uendelezaji wa biashara kama vile Brella, TRA, Afisa Biashara, Wakala wa Vipimo, taasisi za kibenki na sekta binafsi inayowakilishwa na Kampuni ya GODTEC. Katikati ni Mwenyekiti wa MKURABITA,Balozi Daniel Ole Njolay na Mratibu wa Mkurabita Bibi Seraphia Mgembe.

Muonekano wa mfumo wa teknolojia utakaotumika katika zoezi zima la urasimishaji.Urasimishaji wa rasilimali na biashara ni nyenzo muhimu ya kuibua na kuwezesha mwananchi kuwa wawekezaji wa ndani na utawafanya wawajibike katika ujenzi wa uchumi wa viwanda.

Mmoja wa watoa huduma katika kituo cha Urasimishaji na Uendelezaji Biashara , Bi. Regina Richard akimpa maelekezo mwananchi aliyefika katika kituo hicho kwa ajili ya kupata huduma ya usajili wa biashara jana Wilayani Bariadi. Vituo hivyo vitakuwa vikitoa huduma za urasimishaji biashara kwa kuwepo wataalamu wote wanaohusika na usajili na utoaji huduma za uanzzishaji na uendelezaji wa biashara kama vile Brella, TRA, Afisa Biashara, Wakala wa Vipimo, taasisi za kibenki na sekta binafsi inayowakilishwa na Kampuni ya GODTEC.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Simiyu ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Bw. Festo Kiswaga akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa MKURABITA na Kampuni ya GODTEC mara baada ya uzinduzi wa Kituo Kimoja cha Kurasimisha na Kuendeleza Biashara kwa Kanda ya Ziwa Mashariki leo Mjini Bariadi. Vituo hivyo vitakuwa vikitoa huduma za urasimishaji biashara kwa kuwepo wataalamu wote wanaohusika na usajili na utoaji huduma za uanzzishaji na uendelezaji wa biashara kama vile Brella, TRA, Afisa Biashara, Wakala wa Vipimo, taasisi za kibenki na sekta binafsi inayowakilishwa na Kampuni ya GODTEC. (Picha zote na: Frank Shija – MAELEZO, Bariadi).

Kutokana na ukweli kwamba urasimishaji wa rasilimali na biashara kuwa nyenzo muhimu ya kuwezesha kuibua na kuendeleza uwezo wa wananchi hususan vijana kuwa wawekezaji wa ndani na kuwafanya wawajibike kutaengeneza mitaji, soko, ajira na kujenga uchumi wa viwanda ndani ya mfumo rasmi Serikali kupitia MKURABITA kwa kushirikiana na  Kampuni binafsi ya kusaidia uendelezaji biashara ya GODTEC Co. Ltd  walibuni mradi huo wa utoaji huduma kupitia kituo kimoja katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa ambapo utekelezaji wake utahusisha MKURABITA, Mamlaka za Serikali za Mitaa, BRELA,TRA, SIDO, Mifuko ya Hifadhi za Jamii, Wakala wa Vipimo (WMA) na baadhi ya sekta binafsi zikiongozwa na GODTEC Co. Ltd,

2 thoughts on “MKURABITA Yasogeza Huduma za Urasimishaji kwa Wananchi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *