Na Benny Mwaipaja, Dar es Salaam
Wakazi wa Jiji la Dodoma na Wilaya za Bahi, Chemba na Chamwino wanatarajia kuondokana na adha ya maji hivi karibuni baada ya Benki ya Maendeleo ya Afrika – AfDB, kutoa mkopo wenye masharti nafuu wa Dola za Marekani milioni 125. 2, sawa na shilingi za Tanzania bilioni 289.34 kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira-Dodoma.
Mkataba wa mkopo huo umesainiwa leo (tarehe 16 Mei 2022) jijini Dar es Salaam na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Dkt Patrician N. Laverley.
Pages: 1 2
stromectol https://ivermectinus.com/