Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Mhe. Kapteni Mstaafu George Mkuchika Azindua Mwongozo wa Utekelezaji wa Shughuli za Ustawi wa Jamii

Na WMJJWM, Dodoma


Akizindua mwongozo huo kwa niaba ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi Maalum, Mhe. Kapteni Mstaafu George Mkuchika amesema, Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa amezitaka Wizara zinazohusika na utekelezaji wa Mwongozo wa Mpango Kabambe wa Afua za Ustawi wa Jamii kuhakikisha zinasimamia urasimishwaji na utekelezaji wa mwongozo huo katika jamii.


Hayo yamebainika wakati wa uzinduzi wa Mwongozo huo uliofanyika leo Septemba 23, 2022 jijini Dodoma ambapo Mhe. Mkuchika ameeleza kuwa utekelezaji wa Afua za Ustawi wa Jamii ni suala mtambuka linalotekelezwa na Wadau tofauti hivyo mwongozo huo utatumiwa na Wadau wa kisekta wanaotoa Huduma za Ustawi katika kuhakikisha Mipango na bajeti zao zinaakisi Mipango na vipaumbele vya Serikali.


“Mwongozo huu pia utasaidia katika upangaji wa Mipango, bajeti pamoja na upatikanaji wa taarifa mbalimbali zinazowahusu watoto, watu wenye ulemavu, wazee na Makundi Maalum” amesema  Mhe. Mkuchika.


 Ameongeza kuwa utekelezaji wa mwongozo huu utachochea kwa kiasi kikubwa kasi ya utoaji na upatikanaji wa Huduma Bora za Ustawi wa Jamii kwa Makundi Maalum na hivyo kujenga mustakabali imara wa Jamii ya kitanzania katika kufikia matarajio yao.


Aidha, Mhe. Mkuchika amesema mwongozo huo utaimarisha mfumo wa ukusanyaji wa takwimu za Huduma za Ustawi wa Jamii na kujumuishwa katika mfumo wa kidijitali wa mipango na taarifa.


Ameziagiza pia Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kukusanya takwimu na kuandaa mipango na bajeti za Ustawi wa Jamii kwa mujibu wa mwongozo huo.

28 thoughts on “Mhe. Kapteni Mstaafu George Mkuchika Azindua Mwongozo wa Utekelezaji wa Shughuli za Ustawi wa Jamii

Leave a Reply to CalvinTerly Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama