Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Mhe. Kapteni Mstaafu George Mkuchika Azindua Mwongozo wa Utekelezaji wa Shughuli za Ustawi wa Jamii


“Mwongozo usimamiwe kikamilifu ili kuwezesha utatuzi wa changamoto mbalimbali zinazoikumba Jamii ikiwemo ukatili wa kijinsia hasa wanawake na watoto, mauaji na matukio ya kujiua katika Jamii na ongezeko la watoto wa mitaani”, alisisitiza Mhe. Mkuchika 


Awali akimkaribisha mgeni rasmi, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima amesema lengo la kuzindua mwongozo huo ni kuimarisha utoaji wa huduma kwa Makundi Maalum ikiwemo wazee, walemavu, watu wenye magonjwa sugu, watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi na makundi mengine yenye mahitaji maalum.


“Kumekuwa na ukatili mwingi unaoendelea kwenye jamii na kazi kubwa inafanywa kuhakikisha wananchi wanaelewa haki zao tofauti na mwanzo, tumeenda mbele zaidi tuna jeshi la jamii linayojulikana kama SMAUJATA, nitoe wito kwa wananchi kujiunga na niwapongeze Maafisa Ustawi wa Jamii na Maendeleo ya Jamii kwa kazi kubwa” amesema Mhe. Dkt. Gwajima.


Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Sinyamule ameshukuru kwa niaba ya watekelezaji wa mwongozo huu na kusema kwamba utakuwa kitendea kazi muhimu kwa wao kufanyia kazi ili kuhakikisha Makundi Maalum yanapata huduma zinazostahili. 

“Nazipongeza Wizara kwa kuanzisha mwongozo huu ambao utaunganisha sekta mbalimbali katika kutatua changamoto za Makundi haya”, amesema Mhe. Sinyamule.


Mwongozo huu unatekelezwa na Wizara Taasisi na wadau mbalimbali wa maendeleo zikiwemo Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Fedha na Mipango, Mambo ya Ndani ya Nchi, Katiba na Sheria, Elimu, Sayansi na Teknolojia na Wizara ya Afya.

28 thoughts on “Mhe. Kapteni Mstaafu George Mkuchika Azindua Mwongozo wa Utekelezaji wa Shughuli za Ustawi wa Jamii

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama