Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Mgogoro wa Ardhi wa eneo la Goba – Kisauke Watatuliwa

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo,  Mhe. Kheri James ametolea maamuzi mgogoro wa  ardhi wa eneo la Goba –Kisauke  katika Mtaa wa Tegeta A uliodumu kwa muda wa miaka  mitano na kuelekeza kuwa eneo hilo libaki kuwa  mali ya Mtaa (kijiji).


Akizungumza na wananchi wa  mtaa huo  wakati wa mkutano wa hadhara wa kutolea maamuzi mgogoro huo  leo julai 19, 2021 alisema, maamuzi  hayo yametolewa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi baada ya kufanya uchunguzi wa madai yaliyowasilishwa na familia ya Tabia Mziwanda na Roman Mosha.


Alisema Tume ya uchunguzi iliyoundwa na serikali kuchunguza mgogoro huo ilibaini kuwa familia ya Tabia  Mziwanda  ambayo ilikuwa ikidai kuwa eneo hilo ni mali yao haikuwa nyaraka zozote zinazo halalisha umiliki wa eneo hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama