Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Mfumuko wa Bei wa Mwezi Desemba 2019 Wabaki Kuwa Asilimia 3.8

 

Kaimu Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii Bi. Ruth Minja akizungumza wakati akitangaza mfumuko wa bei wa mwezi Desemba 2019.

Na Mwandishi Wetu

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Desemba, 2019 umebaki kuwa asilimia 3.8 kama ilivyokuwa  mwezi Novemba, 2019.

Akizungumza na waandishi wa habari  leo Jijini Dodoma wakati akiwasilisha taarifa ya hali ya mfumuko wa bei, Kaimu mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii Bi Ruth Minja amesema kuwa mfumuko wa Bei wa mwezi Desemba, 2019 umebaki kuwa sawa kama ilivyokuwa mwezi Novemba,2019 hali iliyochangiwa na kuongezeka na kupungua kwa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula kwa kipindi kilichoishia  Desemba, 2019 ikilinganishwa na mwezi Desemba 2018.

“Baadhi ya bidhaa za vyakula zilizoongezeka bei kwa mwezi Desemba, 2019 zikilinganishwa na bei za mwezi Desemba 2018 ni pamoja na;mchele asilimia 7.0, mtama kwa asilimia 3.3, nyama kwa asilimia 2.3, maharage asilimia 7.7, na viazi mviringo kwa asilimia 2.7”; alisisitiza Minja

Akifafanua amesema kuwa bidhaa zisiszo za vyakula  kwa mwezi  Desemba 2019zilipungua bei ikilinganishwa na mwezi Desemba, 2018, Bidhaa hizo ni pamoja na gesi ya kupikia kwa asilimia 2.1, mafuta ya taa kwa asilimia 7.1,jiko la kupikia la gesi kwa asilimia 1.6, mafuta ya petrol I asilimia 8.7 na dizeli asilimia 8.7.

Mfumuko wa Bei wa bidhaa za Vyakula na Vinywaji Baridi kwa mwaka unaoishia mwezi Desemba, 2019 umeongezeka kwa asilimia 6.3 kutoka asilimia 6.1 kwa mwaka unaoishia mwezi Novemba, 2019.

Aidha, Mfumuko wa Bei wa Taifa kutoka mwezi Januari 2019, umepungua hadi  asilimia 3.4 mwaka 2019 kutoka asilimia 3.5 mwaka 2018.

Kwa upande mwingine, Wastani wa Mfumuko wa Bei wa Bidhaa zisizo za vyakula kwa mwaka 2019 ulipungua hadi asilimia 4.0 kutoka asilimia4.3 ilivyokuwa mwaka 2018.

Kwa upande wa nchi ya Kenya mfumuko wa Bei kwa mwezi Desemba, 2019 umeongezeka hadi asilimia 5.82 kutoka asilimia 5.56 kwa mwaka ulioishia mwezi  Novemba,2019, Wakati nchini Uganda kwa mwezi unaoishia Desemba,2019 mfumuko wa bei umeongezeka hadi asilimia 3.6 kutoka asilimia 3.0 kwa mwaka unaoishia mwezi Novemba 2019.

 

185 thoughts on “Mfumuko wa Bei wa Mwezi Desemba 2019 Wabaki Kuwa Asilimia 3.8

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama