Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Mfumo wa Udhibiti Ubora wa Takwimu za Rasilimali za Maji Kutumika Nchini

Mkurugenzi wa Huduma za Sheria Wizara ya Maji, Simon Nkanyemka amesema Serikali imeanza rasmi matumizi ya mfumo wa uthibiti ubora wa takwimu za rasilimali za maji –Quality Management System (QMS) kwa lengo la kuboresha utendaji kazi wa bodi za maji za mabonde nchini.

Nkanyemka amesema mfumo huo umeanza kutumika rasmi Julai Mosi, 2022 na kila Bodi ya Maji ya Bonde inaendelea kutoa taarifa ya utekelezaji wake wa kila wiki. Nkanyemka ameyasema hayo wakati akihitimisha mafunzo Quality Management (QMS) yalioandaliwa na Wizara ya Maji kwa kushirikiana na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) pamoja na Shirika la Kimataifa la Ujerumani (GiZ) yaliyofanyika jijini Dodoma.

Akihitimisha mafunzo hayo kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji, amesema kuwa lengo kuu la mafunzo ya QMS ni kuboresha utendaji wa shughuli ya msingi za mabonde ya usimamizi na uendelezaji wa rasilimali za maji kwa kutumia takwimu sahihi za wingi na ubora zitakazofanikisha kutimiza malengo ya Serikali ya muda mfupi, kati na mrefu.

One thought on “Mfumo wa Udhibiti Ubora wa Takwimu za Rasilimali za Maji Kutumika Nchini

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama