Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Mawaziri wa Mambo ya Nje, Mawaziri wa Ulinzi wa SADC Wakutana Kujadili Hali ya Amani DRC

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi akifungua mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje pamoja na Mawaziri wa Ulinzi na vyombo vya ulinzi na usalama vya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) Jijini Dar es Salaam

Na: Mwandishi Wetu

Mawaziri wa Mambo ya nchi za Nje pamoja na Mawaziri wa Ulinzi na vyombo vya ulinzi  vya Jumuiya ya Maendeleo  Kusini mwa Afrika (SADC) ijulikanao kama DOUBLE TROIKA wamekutana kwa dharura kujadili hali ya kisasa na amani katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ili kuweka mikakati ya kuendelea kuimarisha amani katika nchi hiy

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo wa dharura wa DOUBLE TROIKA inayojumuisha Troika ya siasa na Troika ya Ulinzi na Usalama, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi amesema kuwa lengo la mkutano huo wa dharura ni kuweka mikakati itakayosaidia kuimarisha amani nchini Congo DRC na kumaliza migogoro inayotishia ustawi wa nchi hiyo iliyodumu kwa miongo mingi.

Katibu Mtendaji wa SADC, Stegomena Taxi akihutubia mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya nchi za Nje pamoja na Mawaziri wa Ulinzi wa vyombo vya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) Jijini Dar es Salaam

Baadhi ya mawaziri pamoja na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama wa vyombo vya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) Jijini Dar es Salaam wakifuatilia mkutano wa Troika

Aidha, Waziri Kabudi amebainisha kuwa mkutano huo utasaidia nchi za SADC zenye vikosi vya ulinzi na usalama nchini DRC yaani Tanzania, malawai na Afrika Kusini kuimarisha amani na DRC kwa kufanya tathmini na kukubaliana hatua za kuchukua ili vita na migogoro ya mara kwa mara inayoibuka Nchini Congo DRC ifikie tamati na amani ya kudumu ipatikane.

“Mkutano huu wa leo ni wa Troika ya Siasa na Troika ya ulinzi na usalama ambapo kupitia mkutano huu tunaamini kuwa tutafanya tathimini ya hali ya amani DRC na kukubaliana ni hatua gani za kuchukua,” amesema Prof. Kabudi

Katika hatua nyingine Prof. kabudi ameongeza kuwa ndani ya mwaka huu amani na demokrasia vimezidi kuimarika katika nchi wanachama wa SADC, kutokana na baadhi ya nchi wanachama kuendesha chaguzi za kidemokrasia zilizomalizika kwa amani katika nchi za Msumbiji na Botswana.

Baadhi ya mawaziri pamoja na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama wa vyombo vya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) Jijini Dar es Salaam wakifuatilia mkutano wa Troika

 

Aidha Prof. Kabudi amesema Tanzania na Nchi 16 wanachama wa SADC bado zinaendelea kupaza sauti kwa jumuiya za kimataifa na nchi ambazo zimeiwekea vikwazo Zimbabwe kuviondoa mara moja kutokana na vikwazo hivyo kutokuwa na uhalali jambo linalosababisha mateso kwa raia wan chi hiyo hususani akina mama na watoto .

“Katika hili la Zimbabwe lazima sisi kama SADC tushikamane na kusafiri pamoja ili tufike kwa umoja wetu” Amesema Prof. kabudi

Awali akitoa hutuba katika mkutano huo, Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika(SADC), Stegomena Taxi amesema kuwa ana matumaini makubwa na mkutano huo unaofanyika jijini Dar es salaam utatathimini na kutoa mapendekezo ya muda mfupi na mrefu kuhusu hali ya usalama, amani na siasa katika nchi ya Congo DRC  na ukanda wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika ili kuhakikisha ukanda huo unakuwa salama na amani

Ameongeza kuwa amani na usalama ni nyenzo mojawapo muhimu katika maendeleo ya kiuchumi na hivyo kupata maendeleo yanayohitajika kwa ajili ya mataifa ya Afrika.

125 thoughts on “Mawaziri wa Mambo ya Nje, Mawaziri wa Ulinzi wa SADC Wakutana Kujadili Hali ya Amani DRC

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *