Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Maudhui ya Redio za Nje ni Lazima Yapitie TCRA – Dkt.Mwakyembe

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akiwa katika kituo cha redio cha Mashujaa Fm ya mkoani Lindi ambapo amefanya mahojiano maalum na kushuhudia makombe iliyopata kituo hicho katika maonyesho ya Nanenane kwa miaka mitatu mfululizo tangu mwaka 2018,ambapo mbali na kutoa pongezi amewataka kufanya kazi kwa weledi na kufuata misingi ya taaluma ya habari  na sheria za nchi

Na Shamimu Nyaki –WHUSM, Lindi.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amesema kwamba Serikali haijazuia maudhui ya redio za nje kusikia nchini bali imeagiza maudhui hayo yapate kibali kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ambayo ndio inayosimamia maudhui ya utangazaji nchini.

Waziri Mwakyembe ameyasema hayo katika mahojiano na redio Mashujaa FM ya mkoani Lindi ambapo amesema kwamba redio za nje zinapaswa kuitaarifu TCRA maudhui inayotaka kurusha, lengo likiwa ni kulinda na kuheshimu maadili ya nchi.

3 thoughts on “Maudhui ya Redio za Nje ni Lazima Yapitie TCRA – Dkt.Mwakyembe

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *