Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Matukio Katika Picha Ziara ya Waziri Mwakyembe Mkoani Singida

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akisoma moja ya kaburi la wakoloni wa Kijerumani eneo la Kilima Tinde wakati akiwa katika ziara ya kikazi katika mkoa wa Singida kwa ajili ya kutembelea maeneo ya historia ya ukombozi wa Bara la Afrika ikiwa ni mikakati ya kuhamasisha viongozi na wananchi kutunza, kuhifadhi na kuyaendeleza maeneo hayo kwa matumizi ya kizazi cha sasa na kijacho.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akiangalia eneo lilotumiwa na wakoloni wa Kijerumani eneo la Kilima Tinde wakati wa ukoloni akiwa katika ziara ya kikazi katika mkoa wa Singida kwa ajili ya kutembelea maeneo ya historia ya ukombozi wa Bara la Afrika ikiwa ni mikakati ya kuhamasisha viongozi na wananchi kutunza, kuhifadhi na kuyaendeleza maeneo hayo kwa matumizi ya kizazi cha sasa na kijacho.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akiangalia handaki lilotumiwa na wakoloni wa Kijerumani eneo la Kilima Tinde wakati wa ukoloni akiwa katika ziara ya kikazi katika mkoa wa Singida kwa ajili ya kutembelea maeneo ya historia ya ukombozi wa Bara la Afrika ikiwa ni mikakati ya kuhamasisha viongozi na wananchi kutunza, kuhifadhi na kuyaendeleza maeneo hayo kwa matumizi ya kizazi cha sasa na kijacho.

73 thoughts on “Matukio Katika Picha Ziara ya Waziri Mwakyembe Mkoani Singida

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama