Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Matukio Katika Picha Uzinduzi wa Wilaya ya Kigamboni

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli akiongea na wananchi baada ya kufungua rasmi majengo ya Mkuu
wa Wilaya ya Kigamboni na la Halmashauri ya Wilaya hiyo na kuizindua
rasmi Wilaya hiyo leo Jumanne Februari 11, 2020

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akiwa na na viongozi wengine akikata utepe kuzindua jengo la Mkuu wa
Wilaya hiyo baada ya kulifungua rasmi leo Jumanne Februari 11, 2020

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Wilaya ya Kigamboni Bw.
Ng’ulwabuzu Ludigija akimpa maelezo kuhusu ujenzi wa jengo la
Halmashauri ya Wilaya hiyo baada ya kulifungua rasmi leo Jumanne
Februari 11, 2020

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkuu wa wilaya ya Kigamboni Mhe. Sarah
Msafiri akiwa na Mkurugenzi wa Wilaya ya Kigamboni Bw. Ng’ulwabuzu
Ludigija na viongozi wengine baada ya kufungua rasmi jengo la
Halmashauri ya Wilaya hiyo baada ya kulifungua rasmi leo Jumanne
Februari 11, 2020

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akiwa na Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo wakiweka saini
vitabu vya wageni katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe
Sarah Msafiri na viongozi wengine baada ya kulifungua rasmi jengo la
ofisi hizo leo Jumanne Februari 11, 2020. Waliosimama ni Mkuu wa Mkoa
wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda na Mkurugenzi wa Wilaya ya
Kigamboni Bw. Ng’ulwabuzu Ludigija

(Picha zote na IKULU)

39 thoughts on “Matukio Katika Picha Uzinduzi wa Wilaya ya Kigamboni

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama