Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Matukio Katika Picha Siku Ya Usalama Na Afya Mahali Pa Kazi-Mbeya.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akipokelewa na watumishi wa OSHA alipowasili katika viwanja vya bustani ya Jiji Mkoani Mbeya kwa ajili ya maadhimisho ya sherehe Usalama na Afya Mahali Pa Kazi yaliyofanyika mkoani hapo kitaifa.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Wenye Ulemavu) Mhe. Stella Ikupa akiweka sahihi kwenye kitabu cha wageni katika banda la maonesho la Wakala wa Afya na Usalama mahala pa Kazi (OSHA) wakati wa maadhimisho hayo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akipewa maelezo ya vifaa saidizi kazini kutoka kwa Mtaalamu kutoka Wakala wa Afya na Usalama Mahala Pa Kazi (OSHA) wakati wa maadhimisho hayo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista pamoja na naibu wake Mhe. Anthony Mavunde wakiangalia mfano wa namna ya kuokoa mtu aliyepata madhara awapo kazini walipotembelea banda la MUST (Mbeya University of Science and Technology) wakati wa kilele cha maadhimisho ya Siku ya Usalama na Afya Mahali Pa Kazi Jijini Mbeya.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista akifurahia pamoja na watumishi wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) baada ya kuibuka washindi wa kwanza kwa kupokea tuzo nyingi kuliko washiriki wengine wa maonesho ya Siku Usalama na Afya Mahali Pa Kazi yaliyofanyika Jijini Mbeya. (PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

129 thoughts on “Matukio Katika Picha Siku Ya Usalama Na Afya Mahali Pa Kazi-Mbeya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama