Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Matukio Katika Picha Siku ya Tatu ya Mafunzo ya Matumizi ya Mfumo wa Epicor 10.2 Jijini Mbeya

Mkufunzi wa Chuo Cha Serikali za Mitaa Hombolo Mkoani Dodoma Bw. Muhsin Danga (kushoto) akisisitiza jambo kwa Mkufunzi wa Chuo hicho Bw. Gration Justuce leo Jijini Mbeya wakati wa mafunzo ya matumizi ya mfumo wa Epicor 10.2 kwa wahasibu, waweka hazina na maafisa ugavi wa mikoa ya Mbeya, Rukwa na Songwe

Sehemu ya Washiriki wa mafunzo ya matumizi ya mfumo wa Epicor 10.2 kwa wahasibu, waweka hazina na maafisa ugavi wa mikoa ya Mbeya, Rukwa na Songwe.

Mshiriki wa mafunzo ya matumizi ya mfumo wa Epicor 10.2 kutoka Halmashuri ya Wilaya ya Busekelo Mkoani Mbeya Bw.Aidan Angettile akifanya mazoezi ya vitendo juu ya namna ya kutumia mfumo wa Epicor 10.2 leo Jijini Mbeya ambapo mafunzo hayo yanaendelea yakiwashirikisha wahasibu, waweka hazina na maafisa ugavi wa Mikoa ya Mbeya, Rukwa na Songwe.

Muhasibu Kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bi.  ASha Msangi akifafanua jambo kwa mmoja wa washiriki wa mafunzo ya matumizi ya mfumo wa Epicor 10.2 yanaoendelea Jijini Mbeya ambapo mafunzo hayo yanaendelea yakiwashirikisha wahasibu, waweka hazina na maafisa ugavi wa Mikoa ya Mbeya, Rukwa na Songwe.

Afisa Usimamizi Fedha, Kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bw. Mmaka Mwinjaka  akitoa maelezo ya namna mfumo wa Epicor 10.2 unavyofanya kazi na utakavyosaidia kuongeza tija  leo Jijini Mbeya ambapo mafunzo hayo yanaendelea yakiwashirikisha wahasibu, waweka hazina na maafisa ugavi wa Mikoa ya Mbeya, Rukwa na Songwe.

Afisa Usimamizi Fedha, Kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bw. Mmaka Mwinjaka  akifafanua jambo kwa washiriki wa mafunzo  ya namna ya kutumia mfumo wa Epicor 10.2 leo Jijini Mbeya ambapo mafunzo hayo yanaendelea yakiwashirikisha wahasibu, waweka hazina na maafisa ugavi wa Mikoa ya Mbeya, Rukwa na Songwe.

 

(Picha zote na Frank Mvungi MAELEZO, Mbeya)

74 thoughts on “Matukio Katika Picha Siku ya Tatu ya Mafunzo ya Matumizi ya Mfumo wa Epicor 10.2 Jijini Mbeya

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama