Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Matukio Katika Picha: Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Mhe. Ally Hassan Mwinyi katika Maadhimisho ya Siku ya Haki za Watoto Duniani.

Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Mhe. Ally Hassan Mwinyi (katikati), akifurahia jambo na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndungulile (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Ally Possi, mara baada ya kuwasili katika Maadhimisho ya Siku ya Haki ya Mtoto Duniani iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere.

Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Mhe. Ally Hassan Mwinyi, baada ya kuwasili katika Sherehe za Kuadhimisha ya Siku ya Haki ya Mtoto Duniani iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere, leo Novemba 20, 2019, ambako alialikwa kuwa mgeni Rasmi.

Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Mhe. Ally Hassan Mwinyi (kulia), akiteta jambo na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndungulile, baada ya kuwasili katika Sherehe za Kuadhimisha ya Siku ya Haki ya Mtoto Duniani iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere, leo Novemba 20, 2019, ambako alialikwa kuwa mgeni Rasmi.

Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Mhe. Ally Hassan Mwinyi, akipata maelezo kutoka kwa mtalaam kutoka Shirika la Watoto Duniani (UNICEF), katika moja ya banda lililokuwepo kwenye Maadhimisho ya Siku ya Haki ya Mtoto Duniani iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndungulile, akizungumza na Washiriki wa Sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Haki ya Mtoto Duniani iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere.

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Ally Possi, akizungumza na Washiriki wa Sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Haki ya Mtoto Duniani iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere.

Mwanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala mwaka wa Tatu, Rose Mweleka, akiwasilisha mada kuhusu jinsi ya kutekeleza haki za watoto wa kike ikiwemo kuwafundisha hatua za makuzi ili kuwawezesha kukabiliana na hali wakifikia umri husika, Mada hiyo iliwasilishwa kwenye Maadhimisho ya Siku ya Haki ya Mtoto Duniani iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere.

Mwakilishi wa Wanafunzi kutoka Zanzibar, Abdulatif Hassan, akiwasilisha mada kuhusu jinsi ya kuwasaidia watu wenye UKIMWI (hasa watoto), ili kuwawezesha kukabiliana na hali bila kuwanyanyapaa, Mada hiyo iliwasilishwa kwenye Maadhimisho ya Siku ya Haki ya Mtoto Duniani iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere.

Wanafunzi wakionyesha bango lenye ujumbe wa haki za watoto mara baada ya kuzindua ajenda kuhusu haki za watoto uliofanyika kwenye Maadhimisho ya Siku ya Haki ya Mtoto Duniani iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere.

Watoto kutoka Shule mbalimbali za Jijini Dar es Salaam, wakiwa kwenye Maadhimisho ya Siku ya Haki ya Mtoto Duniani iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere.

Watoto kutoka Shule mbalimbali za Jijini Dar es Salaam, wakiwa katika picha ya pamoja na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Mhe. Ally Hassan Mwinyi, na viongozi wengine wa Serikali katika Maadhimisho ya Siku ya Haki ya Mtoto Duniani iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere.

Watoto kutoka Kikundi cha Safi Theater cha Jijini Dar es Salaam, wakionesha jinsi watoto wa shule wanavyofanyiwa ukatili wa kijinsia na waendesha Bodaboda na Daladala na kukatishwa masomo, igizo lilitolewa katika Maadhimisho ya Siku ya Haki ya Mtoto Duniani iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere.

Mtoto kutoka Jijini Dar es Salaam, akifuatilia mjadala kuhusu haki za watoto katika Maadhimisho ya Siku ya Haki ya Mtoto Duniani iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere.

30 thoughts on “Matukio Katika Picha: Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Mhe. Ally Hassan Mwinyi katika Maadhimisho ya Siku ya Haki za Watoto Duniani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama