Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Matukio Katika Picha Ofisi ya Waziri Mkuu Yahamia Rasmi Mji wa Serikali Jijini Dodoma

Katibu Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge) Bi. Maimuna Tarishi akiwa anatekeleza majukumu yake katika Ofisi yake Mpya iliyopo katika Mji wa Serikali Kata ya Mtumba, Jijini Dodoma ikiwa ni kutekeleza agizo la Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli alilolitoa tarehe 13 Aprili, 2019.

Mkurugenzi wa Uwekezaji, Bw. Joseph Mramba (katikati) akieleza jambo kwa Katibu Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge) Bi. Maimuna (hayupo pichani) juu ya utayari wa kutekeleza majukumu yao wakati wa kikao hicho kilichofanyika Aprili 15, 2019 katika Mji wa Serikali, Jijini Dodoma.

Katibu Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge) Bi. Maimuna Tarishi akizungumza na baadhi Wakuu wa Idara na Vitengo wakati alipofanya kikao cha kuwakaribisha katika ofisi zao mpya zilizopo katika Mji wa Serikali Aprili 15, 2019.

Muonekano wa jengo la Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) iliyopo katika Mji wa Serikali uliopo Kata ya Mtumba, Jijini Dodoma.

Afisa Mipango Miji wa Jiji la Dodoma, Bw. William Alfayo (wa tatu kutoka kulia) akiwaonesha baadhi ya Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu waliombatana na Katibu Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge) Bi. Maimuna Tarishi (wa pili kutoka kushoto) maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi za Balozi katika Mji huo.

Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali Watu kutoka Wizara ya Madini, Bw. Msajigwa Kabigi (wa pili kutoka kulia) akimpa taarifa Katibu Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge) Bi. Maimuna Tarishi (katikati) juu ya zoezi la kuamishia ofisi zao rasmi katika Mji huo wa Serikali uliopo Kata ya Mtumba, Jijini Dodoma.

Katibu Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge) Bi. Maimuna Tarishi akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi ya Naibu waziri wa Madini iliyopo katika Mji wa Serikali alipotembelea Wizara hiyo ambayo tayari imekwisha hamia Mji wa Serikali.

Katibu Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge) Bi. Maimuna Tarishi akiwa kwenye picha ya pamoja na Watumishi wa Ofisi yake baada ya kumaliza majukumu yao kwa siku ya kwanza katika Ofisi zao mpya zilizopo katika Mji wa Serikali.

One thought on “Matukio Katika Picha Ofisi ya Waziri Mkuu Yahamia Rasmi Mji wa Serikali Jijini Dodoma

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama