Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Matukio Katika Picha: Mkutano wa Waandisi wa Habari TCAA na TAA Miaka Minne ya Rais Magufuli.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Anga (TCAA), Hamza Johari, akifafanua jambo kwa Waandsishi wa Habari (Hawapo pichani), kuhusu Mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Tano kwa miaka minne madarakani ikiwemo ununuzi wa Rada 4 za kuongozea ndege, Mkutano huo na Waandishi wa Habari ulifanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Anga (TCAA), Hamza Johari, akifafanua jambo kwa Waandsishi wa Habari, kuhusu Mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Tano kwa miaka minne madarakani ikiwemo ununuzi wa Rada 4 za kuongozea ndege na kuimarisha Chuo cha Wataalamu wa Kuongoza ndege kilichopo JNIA, Mkutano huo na Waandishi wa Habari ulifanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Idara ya Uhandisi na Huduma za Ufundi kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mbila Mdemu, Akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Tano, ikiwemo ukarabati na ujenzi wa Viwanja vya ndege, Mkutano huo na Waandishi wa Habari ulifanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Meneja Mipango na Takwimu kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Asteria Mushi akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari (Hawapo Pichani) kuhusu mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Tano, ikiwemo ukarabati na ujenzi wa Viwanja vya ndege, Mkutano huo na Waandishi wa Habari ulifanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Kaimu Mwanasheria kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Pamela Mugarula akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani), kuhusu mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Tano, ikiwemo ukarabati na ujenzi wa Viwanja vya ndege, Mkutano huo na Waandishi wa Habari ulifanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama