Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Matukio katika picha: Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji Sekta ya Madini Tanzania 2020 JNICC, DSM.

Waziri wa Madini, Mhe. Doto Biteko akizungumza na washiriki wa Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini Tanzania 2020, unaoendelea katika Kituo cha Mikutano Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, alipowasili kufungua Mkutano huo ambapo Tanzania inatarajia kuzindua cheti cha uhalisia ili kuwezesha usafirishaji wa Madini ya Bati.

Naibu Waziri wa Madini, Mhe. Stanslaus Nyongo akizungumza na washiriki wa Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini Tanzania 2020, uliofanyika katika Kituo cha Mikutano Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, ambapo Tanzania inatarajia kuzindua cheti cha uhalisia ili kuwezesha usafirishaji wa Madini ya Bati.

Waziri wa Madini wa Uganda, Mhe. Sara Opendi, akizungumza na washiriki wa Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini Tanzania 2020, uliofanyika katika Kituo cha Mikutano Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, ambapo Tanzania inatarajia kuzindua cheti cha uhalisia ili kuwezesha usafirishaji wa Madini ya Bati.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof.Simon Msanjira akitoa utambulisho wa Viongozi na Wageni mbalimbali kutoka mataifa waliohudhuria Mkutano wa Uwekezaji wa Madini Tanzania 2020 uliofanyika katika Kituo cha Mikutano Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, ambapo Tanzania inatarajia kuzindua cheti cha uhalisia ili kuwezesha usafirishaji wa Madini ya Bati.

Rais wa Chama cha Wachimbaji wa Madini(FEMAT), Bw.John Bina akitoa taarifa ya chama hicho katika Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji wa Madini Tanzania 2020 uliofanyika katika Kituo cha Mikutano Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, ambapo Tanzania inatarajia kuzindua cheti cha uhalisia ili kuwezesha usafirishaji wa Madini ya Bati.

Mmoja wa watoa Maada kuhusu madini katika Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji wa Madini Tanzania 2020, ambaye pia ni Kamishina wa Tume ya Madini, Prof.Abdulkarim Mruma akizungumza katika mkutano huo uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, Februari 22, 2020.

Kutoka kushoto Waziri wa Madini, Mhe. Doto Biteko, Waziri wa Madini wa Uganda, Mhe. Sara Opendi, Balozi Ambeyi Ligabo, Naibu Waziri Madini, Mhe. Stanslaus Nyongo na Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wa Madini(TAMIDA), Bw.Sammy Mollel wakifuatilia Makala kuhusu sekta ya Madini Tanzania iliyooneshwa katika Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji wa Madini Tanzania 2020 uliofanyika katika Kituo cha Mikutano Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, ambapo Tanzania inatarajia kuzindua cheti cha uhalisia ili kuwezesha usafirishaji wa Madini ya Bati.

Waziri wa Madini, Mhe. Doto Biteko akiteta jambo na Waziri wa Madini wa Uganda, Mhe. Sara Opendi, mara baada ya kufungua Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji Sekta ya Madini Tanzania 2020, uliofanyika katika Kituo cha Mikutano Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, ambapo Tanzania inatarajia kuzindua cheti cha uhalisia ili kuwezesha usafirishaji wa Madini ya Bati.

Waziri wa Madini, Mhe. Doto Biteko na Viongozi wengine Washiki wa Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji Sekta ya Madini Tanzania 2020, wakifuatilia Mkutano huo katika Kituo cha Mikutano Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo Februari 22, 2020.

Washiriki wa Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji Sekta ya Madini Tanzania,2020 (Pichani) wakifuatilia Mkutano huo uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam.

102 thoughts on “Matukio katika picha: Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji Sekta ya Madini Tanzania 2020 JNICC, DSM.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama