Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Matukio Katika Picha Mazishi ya Marehemu Sagati Wilayani Bunda

Sehemu ya waombolezaji waliofika kushiriki katika mazishi ya marehemu Shadrack Sagati ambaye alikuwa Afisa Habari Mwandamizi wa Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji wakifuatilia ibada ya mazishi yaliyofanyika jana kijijini kwao Mwiruruma, Bunda mkoani Mara.

Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari MAELEZO Bi. Zamaradi Kawawa akitoa salamu za pole kwa niaba ya Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo kwa familia ya marehemu Shadrack Sagati ambaye alikuwa Afisa Habari Mwandamizi wa Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji wakati wa ibada ya mazishi iliyofanyika kijijini kwao Mwiruruma Wilayani Bunda, mkoani Mara mapema jana.

Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Viwanda  Biashara na Uwekezaji Bi. Emma Lyimo akitoa pole kwa familia ya marehemu Shadrack Sagati ambaye alikuwa Afisa Habari Mwandamizi wa Wizara hiyo wakati wa Ibada ya mazishi iliyofanyika kijijini kwao Mwiruruma Wilayani Bunda, mkoani Mara mapema jana.

Mwakilishi wa Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) Bi. Gaudensia Simwanza akitoa salamu za pole kwa familia ya marehemu Shadrack Sagati ambaye alikuwa Afisa Habari Mwandamizi wa Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji wakati wa Ibada ya mazishi iliyofanyika kijijini kwao Mwiruruma Wilayani Bunda,  mkoani Mara mapema jana.

Waombolezaji wakielekea katika viwanja vya makaburi ya familia ya marehemu Shadrack Sagati ambaye alikuwa Afisa Habari Mwandamizi wa Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji mara baada ya ibada ya mazishi  yake iliyofanyika kijijini kwao Mwiruruma Wilayani Bunda,  mkoani Mara mapema jana.

Mzee wa Kanisa la Kisabato Usharika wa Mwiruruma Wilayani Bunda Mkoani Mara Bw. John Taitus akitoa mahubiri wakati wa ibada ya mazishi  ya marehemu Shadrack Sagati ambaye alikuwa Afisa Habari Mwandamizi wa Wizara ya Viwanda Biashara ambaye alifariki hivi karibuni kwa ajali, ibada ya mazishi  yake iliyofanyika kijijini kwao Mwiruruma Wilayani Bunda, mkoani Mara mapema jana.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara  Tanzania (TAnTRADE) Bw. Edwin Rutageruka akitoa pole  kwa  Bi. Cesilia Sagati ambaye ni mjane wa marehemu Shadrack Sagati wakati wa  kuaga mwili wa marehemu kabla ya kuzikwa kijijini kwao Mwiruruma Wilayani Bunda mapema jana.

Mjane wa marehemu  Shadrack Sagati ambaye alikuwa Afisa Habari Mwandamizi wa Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji (Katikati) Bi. Cesilia Sagati  akiwa kwenye ibada ya kuaga mwili wa marememu mume wake Kijijini kwao Mwiruruma Wilayani Bunda, mkoani Mara kabla ya mazishi yaliyofanyika katika makaburi ya familia Kijijini hapo.

Wawakilishi wa Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO)wakiongozwa na Bi. Gaudensia Simwanza (kushoto) wakiweka shada la maua kwenye kaburi la aliyekuwa Afisa Habari Mwandamizi wa Wizara ya Viwanda Biashara  na Uwekezaji ambaye alifariki hivi karibuni kwa ajali, ibada ya mazishi   iliyofanyika kikijini kwao Mwiruruma Wilayani Bunda mapema jana.

Mjane wa marehemu marehemu Shadrack Sagati ambaye alikuwa Afisa Habari Mwandamizi wa Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji (Katikati) Bi. Cesilia Sagati  akiweka shada la maua kwenye kaburi  wakati wa ibada ya mazishi iliyofanyika kijijini Mwiruruma, Wilayani Bunda mkoani Mara jana.

Mwili wa marehemu Shadrack Sagati ambaye alikuwa Afisa Habari Mwandamizi wa Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji ukiwekwa kaburini mara baada ya ibada ya mazishi iliyofanyika katika Kijiji cha  Mwiruruma Wilayani Bunda Mkoani Mara jana.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara  Tanzania (TAnTRADE) Bw. Edwin Rutageruka akitoa salamu za pole kwa familia ya marehemu Shadrack Sagati wakati mazishi yaliyofanyika Kijijini kwao Mwiruruma, Bunda mkoani Mara jana.

Sehemu ya waombolezaji wakishindwa kuzuia hisia zao wakati wa ibada ya kuaga mwili wa marehemu Shadrack Sagati ambaye alikuwa Afisa Habari Mwandamizi wa Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji kabla ya kuzikwa kijijini kwao Mwiruruma, Bunda mkoani Mara.

 Sehemu ya Wanatasnia ya Habari  na Mawasiliano wakiwa kwenye picha ya pamoja na mjane wa maremu Shadrack Sagati  Bi. Cesilia Sagati (watano kutoka kulia) mara baada ya mazishi yaliyofanyika jana Kijijini kwao Mwiruruma, Bunda mkoani Mara.

Waombolezaji pamoja na ndugu jamaa na marafiki wakijiandaa kuweka mwili wa marehemu Shadrack Sagati  kaburini mara baada ya ibada ya mazishi yaliyofanyika jana kijijini kwao Mwiruruma, Bunda mkoani Mara.

(Picha na Frank Mvungi- MAELEZO, Mara)


FacebooktwittermailFacebooktwittermail