Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Matukio katika Picha Mafunzo ya Kuwajengea uwezo Maafisa Utumishi na Wataalamu wa Afya wa Halmashauri za mkoa wa Ruvuma Juu ya namna Bora ya Upangaji wa Watumishi Katika vituo vya Kutolea Huduma

Bi Restituta Masao mmoja kati ya wawezeshaji wa mafunzo kwa maafisa utumishi wa mkoa wa Dar es sallam akitoa elimu kwa washiriki wa mafunzo ya kuwajengea uwezo maafisa utumishi na wataalamu wa afya wa halmashauri za mkoa  huo juu ya namna bora ya upangaji wa watumishi katika vituo vya kutolea huduma kwa kuzingatia mahitaji.Mwezeshaji wa mafunzo ya WISN PLUS POA ,Joram Kiungo toka Tamisemi akitoa somo kwa washiriki wa mkoa wa Dar jinsi ya utoaji wa taarifa za kimfumo katika upangaji wa watumishi katika halmashauri zao Mafunzo ya siku mbili yaliyoanza leo mkoani mtwara na kufanyika katika kanda 6 Nchini na kusimamiwa na tamisemi kupitia mradi wa uboreshaji wa mifumo ps 3 chini ya ufadhili wa USAID.

Mwenyekiti wa mafunzo ya WISN PLUS POA Kwa mkoa wa Dar es salaam ambae pia ni Afisa Utumishi wa halmashauri ya manispaa ya kigamboni,Wensenclaus Lindi  akiongoza washiriki wake katika mafunzo hayo ya siku mbili mjini Mtwara.

Meneja mradi wa Ps3 Mkoa wa Lindi Aloyce Mwasuka akifafanua jambo kwa  washiriki wa mafunzo hayo ya siku mbili kwa mkoa wa Dar es sallam katika siku ya kwanza ya mafunzo hayo kwa halmashauri zote za mkoa wa Dar es sallam baada ya mkoa wa Lindi kumaliza jana katika ukumbi wa klabu ya bandari manispaa ya mtwara hii leo

Mwezeshaji wa mafunzo ya Wisn plus Poa ,Bi Christina Godfrey ,ambae ni afisa program ,sera  na uraghibishi PS 3  akitoa elimu juu matumizi ya Tehama ikiwa ni  kuwajengea uwezo maafisa utumishi na wataalamu wa afya wa halmashauri za mkoa wa Ruvuma juu ya namna bora ya upangaji wa watumishi katika vituo vya kutolea huduma kwa kuzingatia mahitaji.

 Mshauri wa rasilimali watu kutoka Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma PS3, Zawadi Dakika, akitoa maelekezo kwa  Zuberi Mshamu afisa rasilimali watu halmashauri ya wilaya ya tunduru mkoani Ruvuma katika  mafunzo ya kuwajengea uwezo maafisa utumishi na wataalamu wa afya wa halmashauri za mkoa wa Ruvuma juu ya namna bora ya upangaji wa watumishi katika vituo vya kutolea huduma kwa kuzingatia mahitaji. Mafunzo hayo ya siku mbili yanafanyika mkoani Mtwara yakiendeshwa na mradi wa PS3 kwa ufadhili wa shirika la misaada la marekani la USAID.

Meneja mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma PS3 mkoa wa Mtwara, Amina Rajabu, pichani akiwa na Bw Peter Henze afisa usafirishaji ps 3 pamoja na Prosper Mbena  dereva wa ps 3 wakiratibu baadhi ya masuala ya kiutawala  katika mafunzo ya kuwajengea uwezo maafisa utumishi na wataalamu wa afya wa halmashauri za mkoa wa Mtwara juu ya namna bora ya upangaji wa watumishi katika vituo vya kutolea huduma kwa kuzingatia mahitaji katika ukumbi wa benki kuu manispaa ya mtwara  chini ya ufadhili wa shirika la Kimarekani la USAID

 

(Picha zote na PS3)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *