Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Matukio Katika Picha Maendeleo ya Ujenzi wa Mji wa Serikali

Katibu wa Kikosi Kazi cha Taifa cha Kuratibu Mpango wa Serikali Kuhamia Dodoma, Bw. Meshach Bandawe akikabidhi fomu za maombi ya kuunganishiwa umeme za Wizara zote kwa Kaimu Meneja wa TANESCO Mkoa wa Dodoma, Mhandisi. Tumaini Nyale walipokutana wakati wa kukagua maendeleo ya ujenzi wa Mji wa Serikali jijini Dodoma leo tarehe 29 Desemba, 2018. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Dkt. Titus Mwinuka.

Katibu wa Kikosi Kazi cha Taifa cha Kuratibu Mpango wa Serikali Kuhamia Dodoma, Bw. Meshach Bandawe akisisitiza jambo mara baada ya kukabidhi fomu za maombi ya kuunganishiwa umeme za Wizara zote kwa Kaimu Meneja wa TANESCO Mkoa wa Dodoma, Mhandisi. Tumaini Nyale (katikati) walipokutana wakati wa zoezi la kukagua maendeleo ya ujenzi wa Mji wa Serikali jijini Dodoma leo tarehe 29 Desemba, 2018.Wapili kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Dkt. Titus Mwinuka na kushoto ni Mkurugenzi wa Uwezeshaji Sekta Binafsi toka Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Bedason Shallanda.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Dkt. Titus Mwinuka (katikati) akisikiliza kwa makini maelekezo toka kwa Katibu wa Kikosi Kazi cha Taifa cha Kuratibu Mpango wa Serikali Kuhamia Dodoma, Bw. Meshach Bandawe walipokutana wakati wa zoezi la kukagua maendeleo ya ujenzi wa Mji wa Serikali jijini Dodoma leo tarehe 29 Desemba, 2018.

Katibu wa Kikosi Kazi cha Taifa cha Kuratibu Mpango wa Serikali Kuhamia Dodoma, Bw. Meshach Bandawe akitoa maelekezo kwa Kaimu Meneja wa TANESCO Mkoa wa Dodoma, Mhandisi. Tumaini Nyale (katikati) mara baada ya kumkabidhi fomu za maombi ya kuunganishiwa umeme za Wizara zote wakati wa zoezi la kukagua maendeleo ya ujenzi wa Mji wa Serikali jijini Dodoma leo tarehe 29 Desemba, 2018. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Dkt. Titus Mwinuka

Katibu wa Kikosi Kazi cha Taifa cha Kuratibu Mpango wa Serikali Kuhamia Dodoma, Bw. Meshach Bandawe (watatu kutoka kushoto) na Mkurugenzi wa Uwezeshaji Sekta Binafsi toka Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Bedason Shallanda (kulia kwake) wakikagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la Ofisi za Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto leo jijini Dodoma.

Katibu wa Kikosi Kazi cha Taifa cha Kuratibu Mpango wa Serikali Kuhamia Dodoma, Bw. Meshach Bandawe (kushoto) akikagua utekelezaji wa agizo la Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Bibi. Maimnua Tarishi (hayupo picha) lilomtaka Mkandarasi anayejenga Ofisi za Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ambaye ni Kikosi cha Ujenzi ambao walitakiwa kufuata muongozo wa Mkandarasi Mshauri ambaye ni TBA leo jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Uwezeshaji Sekta Binafsi toka Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Bedason Shallanda akifafanua jambo wakati wa ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa Ofisi ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano leo jijini Dodoma. Aliyevaa tisheti ni Katibu wa Kikosi Kazi cha Taifa cha Kuratibu Mpango wa Serikali Kuhamia Dodoma, Bw. Meshach Bandawe.

Katibu wa Kikosi Kazi cha Taifa cha Kuratibu Mpango wa Serikali Kuhamia Dodoma, Bw. Meshach Bandawe akielezea jambo alipokuwa akikagua maendeleo ya utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa la kuitaka TBA kuwa na Ofisi katika eneo unapojengwa Mji wa Serikali ili kuharakisha huduma za ushauri kwa Makandarasi wanaoendelea na ujenzi wa Ofisi za Wizara mbalimbali leo jijini Dodoma. Kushoto ni Mkurugenzi wa Uwezeshaji Sekta Binafsi toka Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Bedason Shallanda.

Katibu wa Kikosi Kazi cha Taifa cha Kuratibu Mpango wa Serikali Kuhamia Dodoma, Bw. Meshach Bandawe (kulia) akielezea jambo wakati wa ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa Ofisi ya Waziri Mkuu ( Sera, Uratibu na Bunge) leo jijini Dodoma.

Katibu wa Kikosi Kazi cha Taifa cha Kuratibu Mpango wa Serikali Kuhamia Dodoma, Bw. Meshach Bandawe (kulia) akielekeza jambo wakati wa ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa leo jijini Dodoma. (Picha zote na: Frank Shija – MAELEZO, Dodoma)

57 thoughts on “Matukio Katika Picha Maendeleo ya Ujenzi wa Mji wa Serikali

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *