
. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma kukagua hatua iliyofikiwa katika maandalizi ya sherehe za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zinazotarajiwa kufanyika tarehe 26 mwezi huu mjini Dodoma.

. Komando wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania wakionesha umahiri wao wakati wa maandalizi ya sherehe za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zinazotarajiwa kufanyika tarehe 26 mwezi huu mjini Dodoma.

Askari wa Jeshi la Magereza, wakionesha zoezi la kupambana na adui mbele Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, wakati alipokagua maandalizi ya sherehe za miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma Aprili 24, 2018.

Mwanamuziki mkongwe hapa nchini Bw. Cosmas Chidumule akitumbuiza kama sehemu ya maandalizi ya sherehe za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zinazotarajiwa kufanyika tarehe 26 mwezi huu mjini Dodoma katika uwanja wa Jamhuri mjini humo.

Wanafunzi wanaounda kikundi cha halaiki wakionesha umahiri wao katika kupambana na adui wakati wa maandalizi ya sherehe za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zinazotarajiwa kufanyika tarehe 26 mwezi huu mjini Dodoma.