Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Matukio Katika Picha Kikao cha Kujadili Ujenzi wa Majengo ya Ofisi za Wizara Awamu ya Pili eneo la Mtumba

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge) Bw. Tixon Nzunda akizungumza neno la ufunguzi wakati wa kikao kazi cha wadau wa ujenzi walipokutana Januari 27, 2020 kujadili mpango kabambe wa Ujenzi wa Ofisi za Wizara Awamu ya Pili katika eneo la Mji wa Serikali Mtumba Dodoma.Kikao kilifanyika katika Ukimbi wa Mkutano wa ofisi yake Dodoma, wa kwanza kushoto ni Katibu wa kikosi kazi cha kuratibu zoezi la Serikali kuhamia Dodoma Bw. Meshack Bandawe.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Arch. Elius Mwakalinga akichangia jambo wakati wa kikao kazi cha wadau wa ujenzi walipokutana Januari 27, 2020 kujadili mpango wa Ujenzi wa Ofisi za Wizara Awamu ya Pili katika eneo la Mji wa Serikali Mtumba Dodoma.

Sehemu ya wajumbe wa kikao cha kujadili mpango kabambe wa ujenzi wa majengo ya ofisi za serikali kwa Awamu ya Pili wakifuatilia hoja za kikao hicho.

Sehemu ya wajumbe wa kikao cha kujadili mpango kabambe wa ujenzi wa majengo ya ofisi za serikali kwa Awamu ya Pili wakifuatilia hoja za kikao hicho.

(Picha zote na Ofisi ya Waziri mkuu)

228 thoughts on “Matukio Katika Picha Kikao cha Kujadili Ujenzi wa Majengo ya Ofisi za Wizara Awamu ya Pili eneo la Mtumba

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama