Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Matukio Katika Picha Hafla ya Kufunga Mafunzo ya Matumizi ya Mfumo wa Malipo ya Serikali kwa njia ya Mtandao.

Mwezeshaji kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Goodluck Mbano akiwasilisha mada kwa wahasibu  na wataalamu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo kuhusu mfumo wa malipo kwa njia ya mtandao  leo Jijini Dodoma.

Mhasibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Stephen Dalasia akisisitiza jambo kwa mmoja wa wahasibu wa Wizara hiyo Bi. Winifrida Method leo Jijini Dodoma wakati wa mafunzo ya mfumo wa malipo ya Serikali kwa njia ya mtandao yaliyofanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo.

Sehemu ya washiriki wa mafunzo  ya mfumo wa malipo ya Serikali kwa njia ya mtandao kutoka Wizara ya Habari  Utamaduni Sanaa na Michezo wakifuatilia mafunzo hayo leo Jijini Dodoma.

Mhasibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Stephen Dalasia akisisitiza jambo kwa  sehemu ya washiriki wa mafunzo  ya mfumo wa malipo ya Serikali kwa njia ya mtandao kutoka Wizara ya Habari wakifuatilia mafunzo hay oleo Jijini Dodoma.

Sehemu ya washiriki wa mafunzo  ya mfumo wa malipo ya Serikali kwa njia ya mtandao kutoka Wizara ya Habari wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya mafunzo hayo  leo Jijini Dodoma.

 Wahasibu wa Wizara ya  Habari Utamaduni Sanaa na Michezo wakifurahia jambo , kutoka kushoto ni Bw Jackson Manyika na kulia ni Bw. Christopher  Raphael.

(Picha zote na Frank Mvungi- MAELEZO)

 


FacebooktwittermailFacebooktwittermail