Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Matukio Katika Picha Bungeni Leo Mei 23, 2019

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akijibu maswali ya papo kwa papo leo Bungeni Jijini Dodoma.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Mwita Waitara akisisitiza kuhusu mikakati ya Serikali kuimarisha huduma za Jamii katika Mamlaka za Serikali za Mitaa leo Bungeni Jijini Dodoma.

Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamis Kigwangala akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2019/2020.

Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii (TTB) Mhe. Jaji Mstaafu Marko Mihayo (wakwanza kushoto) akiwa Bungeni leo Jijini Dodoma kabla ya kuwasilishwa kwa Bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii.

Spika wa Bunge La Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akisisitiza jambo mara baada ya kipindi cha maswali na majibu.

Mbunge wa Babati Mjini Mhe. Pauline Gekulu akisisitiza jambo Bungeni wakati wa kipindi cha maswali na majibu leo.

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Walemavu Mhe. Stella Ikupa akiwa kwenye picha ya pamoja na Timu ya Tembo Worriors waliofika Bungeni leo ikiwa ni sehemu ya uhamasishaji wananchi na wabunge kushiriki katika maandalizi na mashindano ya mpira wa miguu kwa wenye ulemavu kwa nchi za Afrika Mashariki yanayotarajiwa kufamnyika hapa nchini hivi karibuni.

Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Elias Kuandikwa akijibu swali Bungeni leo.

(Picha zote na Frank Mvungi)

52 thoughts on “Matukio Katika Picha Bungeni Leo Mei 23, 2019

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama