Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Matukio katika Picha Bungeni Leo Aprili 24, 2019

Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamis Kigwangala akisisitiza jambo kwa Waziri wa Fedha na Mipango leo Bungeni Jijini Dodoma.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akimsikiliza Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Omary Mgumba leo Bungeni Jijini Dodoma.

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akisisitiza kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuhakikisha kuwa haki za watoto zinalindwa ikiwemo kuwalinda dhidi ya vitendo vya udhalilishaji leo Bungeni Jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu akieleza hatua zilizofikiwa na Serikali katika kuhakikisha kuwa wananchi wote wanafikiwa na nishati ya umeme katika maeneo yote ya Vijijini na mijini ambayo hayajafikiwa na nishati hiyo.

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akisisitiza jambo mara baada ya kipindi cha maswali na majibu Bungeni Jijini Dodoma.

. Sehemu ya wageni waliofika Bungeni wakifuatilia kipindi cha maswali na majibu Bungeni leo akiwemo Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa NMB Bi. Magreth Ikongo (wapili kutoka kulia) hayo yamejiri Bungeni Jijini Dodoma.

Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamis Kigwangala na Naibu wake Mhe. Costantine Kanyasu (kulia) wakifuatilia hoja za wabunge leo Bungeni wakati wakichangia hoja ya bajeti ya Wizara hiyo leo Bungeni Jijini Dodoma.

(Picha zote na Frank Mvungi)

127 thoughts on “Matukio katika Picha Bungeni Leo Aprili 24, 2019

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama