Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Matukio ya Bunge katika Picha

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akimweleza jambo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa, wakati wa Mkutano wa Bunge la Kumi na Moja wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo Mjini Dodoma.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harisson Mwakyembe akiteta jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (kulia) na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza wakati wa Mkutano wa Bunge la Kumi na Moja la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, elo Mjini Dodoma.

Naibu Waziri Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Mhandisi Stella Manyanya akijibu maswali ya wabunge, wakati wa Mkutano wa Bunge la Kumi na Moja la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo Mjini Dodoma.

 

Naibu Waziri Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. William Ole Nasha akijibu hoja za wabunge, wakati wa Mkutano wa Bunge la Kumi na Moja la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo Mjini Dodoma.

 

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akiongoza Mkutano wa Bunge la Kumi na Moja la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo Mjini Dodoma.

One thought on “Matukio ya Bunge katika Picha

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *