Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

MATUKIO KATIKA PICHA BUNGENI LEO

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akiwasilisha  hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Fedha  kwa Wizara hiyo kwa mwaka 2018/19  Bungeni mjini Dodoma mapema leo.

Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu akitoa maelezo Bungeni  mapema leo kuhusu mikakati ya Serikali kuhusu kufikisha umeme katika vijiji vyote hapa nchini.

Mbunge wa Mwanga Prof. Jumanne Maghembe akichangia hoja ya  Bajeti ya Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia kuhusu mikakati inayoweza kusaidia kuendelea kukuza kiwango cha elimu hapa nchini.

Naibu Waziri wa  Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano  Mhe. Elias Kuandikwa akijibu swali Bungeni  mjini Dodoma kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kujenga miundo mbinu  hapa nchini.

Wageni mbalimbali walihudhuria Bunge wakiwemo Skauti  wakifuatilia kipindi cha maswali na majibu mapema leo Bungeni mjini Dodoma.

Naibu  Waziri wa Fedha Dkt. Ashatu Kijaji akisisitiza jambo kwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe leo mjini Dodoma.


FacebooktwittermailFacebooktwittermail