Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Matukio Katika Picha Bungeni Leo

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akijibu swali wakati wa Kikao cha Tisa cha Mkutano wa 15 wa Bunge leo jijini Dodoma.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mwita Waitara akifafanua jambo wakati wa kipindi cha maswali na majibu wakati wa Kikao cha Tisa cha Mkutano wa 15 wa Bunge leo jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye akifafanua jambo wakati wa kipindi cha maswali na majibu wakati wa Kikao cha Tisa cha Mkutano wa 15 wa Bunge leo jijini Dodoma.

Mbunge wa Jimbo la Busanda mkoani Geita, Rolencia Bukwimba akiuliza swali wakati wa kipindi cha maswali na majibu wakati wa Kikao cha Tisa cha Mkutano wa 15 wa Bunge leo jijini Dodoma.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akiteta jambo na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi wakati wa Kikao cha Tisa cha Mkutano wa 15 wa Bunge leo jijini Dodoma.

Baadhi ya wageni wakifuatilia shughuli za Bunge wakati wa Kikao cha Tisa cha Mkutano wa 15 wa Bunge leo jijini Dodoma.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akimsikiliza Mtanzania aliyeshiriki kutunga wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Bw. John Joseph Mugango(kushoto) alipomtembelea Bunge leo jijini Dodoma. Kulia ni Mtoto wa Mtunzi huyo Bi. Joanitha Mugango.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akisalimiana na baadhi ya wahitimu wa Vyuo Vikuu kutoka Mafinga wilayani Mufindi ambao wamejiari wenyewe walipotembelea Bungeni leo jijini Dodoma.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya Maudhui na baadhi ya watendaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) leo Bungeni jijini Dodoma. (Frank Shija – MAELEZO).


FacebooktwittermailFacebooktwittermail