Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Matukio Katika Picha Bungeni Leo

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo pamoja na Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejeimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mary Mwanjelwa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mwita Waitara wakifuatilia michango ya wabunge wakati wa kuchangia Bajeti ya Wizara TAMISEMI ya Mwaka wa Fedha 2019/2020 leo Bungeni jijini Dodoma.

Mbunge wa kuteuliwa Mhe. Salma Kikwete akichangia hoja wakati wa mjadala wa kuchangia Bajeti ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora leo Bungeni jijini Dodoma.

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Mariam Kisiga akichangia hoja wakati wa mjadala wa kuchangia Bajeti ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora leo Bungeni jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu akiteta jambo na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Juliana Shonza wakati wa kikao cha nane cha Mkutano wa 15 wa Bunge leo jijini Dodoma.

Baadhi ya wanafunzi kutoka Chuo cha Uongozi wa Mahakama (IJA) kutoka Tanga wakifuatilia shughuli za Bunge wakati wa kikao cha nane cha Mkutano wa 15 wa Bunge leo jijini Dodoma.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akiteta jambo na Mkurugenzi wa Taasisi ya Arise Amka Afika ya jijini Arusha, Bi. Kuluthum Maabad alipomtembelea Bunge leo jijini Dodoma. Taasisi ya Arise Amka Afrika inajishughulisha na masuala ya utoaji elimu kuhusu harakati za ukombozi wa Bara la Afrika. (Picha na: Frank Shija – MAELEZO)


FacebooktwittermailFacebooktwittermail