Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Matukio Katika Picha Bungeni Leo

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI, akiwasilisha Bajeti ya Wizara yake kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 leo jijini Dodoma.

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson akizungumza katika kikao cha saba cha Mkutano wa 15 wa Bunge leo jijini Dodoma.

Waziri wa Katiba na Sheria Balozi, Dkt. Agustine Mahiga akijibu swali wakati wa kikao cha saba cha Mkutano wa 15 wa Bunge leo jijini Dodoma.

Baadhi ya wafanyakazi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakifuatilia Bunge leo jijini Dodoma wakati Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI na Ofisi ya Rais – Utumishi zikiwasilisha Bajeti zao za Mwaka wa Fedha 2019/2020.

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega wakitoka katika ukumbi wa Bunge leo jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Juliana Shonza akisoma kitabu cha Mashujaa wa Afrika “Afrikan Heroes” kilichoandikwa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Arise Amka Afrika ya jijini Arusha, Bi. Kuluthum Maabad alipotembelea Bungeni leo . Arise Amka Afrika ni Taasisi inayojihusisha na masula ya utoaji elimu kuhusu harakati za Ukombozi wa Bara la Afrika.

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Juliana Shonza (kushoto)na Mkurugenzi wa Taasisi ya Arise Amka Afrika ya jijini Arusha, Bi. Kuluthum Maabad wakifurahia kitabu cha Mashujaa wa Afrika “Afrikan Heroes” kilichoandikwa na Mkurugenzi huyo mara baada ya kumpokea mgeni huyo kwaniaba ya Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe bungeni leo . Arise Amka Afrika ni Taasisi inayojihusisha na masula ya utoaji elimu kuhusu harakati za Ukombozi wa Bara la Afrika. (Picha na: Frank Shija – MAELEZO)

74 thoughts on “Matukio Katika Picha Bungeni Leo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *